Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

2 Wafalme 25:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

27 Ikawa katika mwaka wa thelathini na saba wa kuhamishwa kwake Yekonia, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na saba ya mwezi, Evil-merodaki, mfalme wa Babeli, katika mwaka wa kwanza wa kutawala kwake, akamwinua kichwa Yekonia, mfalme wa Yuda, akamtoa gerezani.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Mnamo mwaka wa thelathini na mbili, Evil-merodaki mfalme wa Babuloni, alipoanza kutawala, mwaka huohuo alimsamehe Yehoyakini mfalme wa Yuda, akamtoa gerezani. Hiyo ilikuwa siku ya ishirini na saba ya mwezi wa kumi na mbili, mwaka wa thelathini na saba tangu Yehoyakini alipochukuliwa mateka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Mnamo mwaka wa thelathini na mbili, Evil-merodaki mfalme wa Babuloni, alipoanza kutawala, mwaka huohuo alimsamehe Yehoyakini mfalme wa Yuda, akamtoa gerezani. Hiyo ilikuwa siku ya ishirini na saba ya mwezi wa kumi na mbili, mwaka wa thelathini na saba tangu Yehoyakini alipochukuliwa mateka.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Katika mwaka wa thelathini na saba tangu Yehoyakini mfalme wa Yuda apelekwe uhamishoni, katika mwaka ule ambao Evil-Merodaki alifanyika mfalme wa Babeli, alimwacha huru Yehoyakini kutoka gerezani siku ya ishirini na saba ya mwezi wa kumi na mbili.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Wafalme 25:27
10 Marejeleo ya Msalaba  

Baada ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako, atakurudisha katika kazi yako; nawe utampa Farao kikombe mkononi mwake, kama desturi ya kwanza, ulipokuwa mnyweshaji wake.

Ikawa siku ya tatu, siku ya kuzaliwa kwake Farao, akawafanyia karamu watumwa wake wote; akakiinua kichwa cha mkuu wa wanyweshaji, na cha mkuu wa waokaji, miongoni mwa watumwa wake.

Na Yekonia, mfalme wa Yuda, akatoka akamwendea mfalme wa Babeli, yeye na mama yake, na watumishi wake, na wakuu wa watu wake, na maofisa wake; mfalme wa Babeli akamchukua mateka katika mwaka wa nane wa kutawala kwake.

Akamchukua Yekonia mpaka Babeli; na mama yake mfalme, na wake zake mfalme, na maofisa wake, na wakuu wa nchi, aliwachukua mateka toka Yerusalemu mpaka Babeli.

Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa BWANA; Kama mifereji ya maji huugeuza popote apendapo.

Nami nitakutupa nje, wewe na mama yako aliyekuzaa, mwende katika nchi nyingine ambayo hamkuzaliwa huko, nanyi mtakufa huko.

Nami nitamrudisha hapa Yekonia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, pamoja na mateka wote wa Yuda, waliokwenda Babeli, asema BWANA; maana nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli.

Ndipo Yeremia akamwambia Sedekia, BWANA, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kama ukitoka kwenda kwa wakuu wa mfalme wa Babeli, basi nafsi yako utaishi, wala mji huu hautateketezwa; nawe utaishi na nyumba yako;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo