Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Wafalme 23:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

7 Akaziangusha nyumba za mahanithi, waliokuwamo nyumbani mwa BWANA, wanawake walipofuma mapazia ya Ashera.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Alibomoa nyumba za mahanithi zilizokuwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, mahali ambamo wanawake walifuma mapazia ya Ashera.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Alibomoa nyumba za mahanithi zilizokuwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, mahali ambamo wanawake walifuma mapazia ya Ashera.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Alibomoa nyumba za mahanithi zilizokuwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, mahali ambamo wanawake walifuma mapazia ya Ashera.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Akabomoa pia nyumba za mahanithi wa mahali pa ibada, zilizokuwa ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu, nyumba ambazo wanawake walifumia pazia kwa ajili ya Ashera.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Akabomoa pia nyumba za mahanithi wa mahali pa ibada za miungu, zilizokuwa ndani ya Hekalu la bwana na mahali wanawake walipofuma kwa ajili ya Ashera.

Tazama sura Nakili




2 Wafalme 23:7
14 Marejeleo ya Msalaba  

Na mahanithi walikuwako katika nchi, wakafanya sawasawa na machukizo yote ya mataifa BWANA aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.


Akawafukuza mahanithi katika nchi, akaziondoa sanamu zote walizozifanya baba zake.


Tena mahanithi waliosalia, hao waliosalia siku za Asa baba yake, akawaondoa katika nchi.


Naye Yosia akayaondolea mbali machukizo yote katika nchi zote zilizokuwa milki ya wana wa Israeli, akawafanya wote walioonekana katika Israeli kutumika, naam, wamtumikie BWANA, Mungu wao. Siku zake zote hawakuacha kumfuata BWANA, Mungu wa baba zao.


Ukatwaa baadhi ya mavazi yako, ukajifanyia mahali palipoinuka, palipopambwa kwa rangi mbalimbali, ukafanya mambo ya kikahaba juu yake; mambo kama hayo hayatakuja wala hayatakuwako.


Ndipo akanileta mpaka maingilio ya lango la kaskazini mwa nyumba ya BWANA, ulioelekea upande wa kaskazini, na tazama, wanawake wameketi wakimlilia Tamuzi.


Nami nitamwadhibu kwa sababu ya siku za Mabaali, aliowafukizia uvumba; hapo alipojipamba kwa pete masikioni mwake, na kwa vito asema BWANA.


Hutoa dhabihu juu ya vilele vya milima, na kufukiza uvumba juu ya vilima, chini ya mialoni na milibua na miela, kwa kuwa uvuli wake ni mwema; kwa sababu hiyo binti zenu huzini, na bibi arusi zenu hufanya uasherati.


Sitawaadhibu binti zenu wazinipo, wala bibi arusi zenu wafanyapo uasherati; maana wenyewe huenda kando pamoja na wanawake wazinzi, hutoa dhabihu pamoja na makahaba; na watu hawa wasiofahamu wataangamia.


Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu;


Pasiwe na kahaba katika binti za Israeli, wala pasiwe na hanithi katika wana wa Israeli wanaume.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo