2 Wafalme 21:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC7 Akaiweka sanamu ya kuchongwa ya Ashera aliyoifanya ndani ya nyumba, ambayo BWANA alimwambia Daudi, na Sulemani mwanawe, Katika nyumba hii, na katika Yerusalemu, niliouchagua miongoni mwa kabila zote za Israeli, nitaliweka jina langu milele; Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema7 Nayo sanamu ya Ashera aliyotengeneza akaiweka katika nyumba ambayo Mwenyezi-Mungu aliizungumzia mbele ya Daudi na mwanawe Solomoni: “Katika nyumba hii na mjini Yerusalemu niliouchagua ndiko mahali nitakapoabudiwa milele. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND7 Nayo sanamu ya Ashera aliyotengeneza akaiweka katika nyumba ambayo Mwenyezi-Mungu aliizungumzia mbele ya Daudi na mwanawe Solomoni: “Katika nyumba hii na mjini Yerusalemu niliouchagua ndiko mahali nitakapoabudiwa milele. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza7 Nayo sanamu ya Ashera aliyotengeneza akaiweka katika nyumba ambayo Mwenyezi-Mungu aliizungumzia mbele ya Daudi na mwanawe Solomoni: “Katika nyumba hii na mjini Yerusalemu niliouchagua ndiko mahali nitakapoabudiwa milele. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu7 Akachukua nguzo ya Ashera aliyoichonga na kuiweka katika Hekalu, ambalo Mwenyezi Mungu alikuwa amemwambia Daudi na mwanawe Sulemani, “Katika Hekalu hili na katika Yerusalemu, mji niliouchagua kutoka makabila yote ya Israeli, nitaliweka Jina langu milele. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu7 Akachukua nguzo ya Ashera aliyoichonga na kuiweka katika Hekalu, ambalo bwana alikuwa amemwambia Daudi na mwanawe Sulemani, “Katika Hekalu hili na katika Yerusalemu niliouchagua kutoka kabila zote za Israeli, nitaliweka Jina langu milele. Tazama sura |
Kisha, mfalme akamwamuru Hilkia, kuhani mkuu, na makuhani wa daraja ya pili, na walinzi wa mlango, kwamba watoe katika hekalu la BWANA vyombo vyote vilivyofanywa kwa ajili ya Baali, na kwa ajili ya Ashera, na kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni; akaviteketeza kwa moto nje ya Yerusalemu, katika mashamba ya Ridroni, akayachukua majivu yake mpaka Betheli.