Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wafalme 21:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

22 Akamwacha BWANA, Mungu wa babaze, wala hakuiendea njia ya BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Alimwacha Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zake, hakushika njia ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Alimwacha Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zake, hakushika njia ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Alimwacha Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zake, hakushika njia ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Akamwacha Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zake, wala hakuenenda katika njia za Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Akamwacha bwana, Mungu wa baba zake, wala hakuenenda katika njia za bwana.

Tazama sura Nakili




2 Wafalme 21:22
9 Marejeleo ya Msalaba  

kwa sababu wameniacha mimi wakaabudu Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni, na Kemoshi, mungu wa Wamoabi, na Milkomu, mungu wa wana wa Amoni wala hawakuenda katika njia zangu, kutenda mema machoni pangu, kuzishika sheria zangu na hukumu zangu, kama Daudi baba yake.


Akaiendea njia yote aliyoiendea baba yake, akazitumikia sanamu alizozitumikia baba yake, akaziabudu.


kwa sababu wameniacha mimi, wameifukizia uvumba miungu mingine, ili wapate kunikasirisha kwa kazi yote ya mikono yao; kwa hiyo hasira yangu itawaka juu ya mahali hapa, isizimike.


Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA huchunguza mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, atakuwa nawe; ukimwacha, atakutupa milele.


Sikieni, enyi mbingu, tega sikio, Ee nchi, kwa maana BWANA amenena; Nimewalisha watoto na kuwalea, nao wameniasi.


Ole wake, taifa lenye dhambi, watu wanaochukua mzigo wa uovu, wazao wa watenda mabaya, watoto wanaoharibu; wamemwacha BWANA, wamemdharau yeye aliye Mtakatifu wa Israeli, wamefarakana naye na kurudi nyuma.


Kwa maana watu wangu hawa wametenda maovu mawili; wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima, wamejichimbia visima, visima vyenye nyufa visivyoweza kuweka maji.


Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo Hujitenga na rehema zao wenyewe.


Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke; Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo