2 Wafalme 19:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC
6 Isaya akawaambia, Mwambieni bwana wenu maneno haya; BWANA asema hivi, Usiyaogope maneno hayo uliyoyasikia, ambayo watumishi wa mfalme wa Ashuru wamenitukana.
6 aliwaambia “Mwambieni bwana wenu kwamba Mwenyezi-Mungu asema hivi, ‘Usiogope kwa sababu ya maneno uliyoyasikia, ambayo watumishi wa mfalme wa Ashuru wameyasema kunikebehi.
6 aliwaambia “Mwambieni bwana wenu kwamba Mwenyezi-Mungu asema hivi, ‘Usiogope kwa sababu ya maneno uliyoyasikia, ambayo watumishi wa mfalme wa Ashuru wameyasema kunikebehi.
6 aliwaambia “Mwambieni bwana wenu kwamba Mwenyezi-Mungu asema hivi, ‘Usiogope kwa sababu ya maneno uliyoyasikia, ambayo watumishi wa mfalme wa Ashuru wameyasema kunikebehi.
6 Isaya akawaambia, “Mwambieni bwana wenu, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Usiogope kwa hayo uliyoyasikia, yale maneno ambayo watumishi wa mfalme wa Ashuru wamenitukana nayo.
6 Isaya akawaambia, “Mwambieni bwana wenu, ‘Hili ndilo asemalo bwana: Usiogope kwa hayo uliyoyasikia, yale maneno ambayo watumishi wa mfalme wa Ashuru wamenitukana nayo.
Mfalme wa Ashuru akawatuma jemadari wake, na mkuu wa matowashi, na kamanda wake, toka Lakishi, kwa mfalme Hezekia huko Yerusalemu, pamoja na jeshi kubwa. Nao wakakwea wakafika Yerusalemu. Na walipokwisha kufika, wakaja wakasimama karibu na mfereji wa birika la juu, lililo katika njia kuu ya kuuendea Uwanda wa Dobi.
akasema, Sikieni, Yuda wote, nanyi mkaao Yerusalemu, na wewe mfalme Yehoshafati; BWANA awaambia hivi, Msiogope, wala msifadhaike kwa ajili ya jeshi kubwa hili; kwani vita si yenu bali ni ya Mungu.
Hamtahitaji kupigana vita, jipangeni, simameni, mkauone wokovu wa BWANA ulio pamoja nanyi, enyi Yuda na Yerusalemu; msiogope, wala msifadhaike; kesho tokeni juu yao; kwa kuwa BWANA yuko pamoja nanyi.
Kwa hiyo Bwana, BWANA wa majeshi, asema hivi, Enyi watu wangu mkaao katika Sayuni, msiogope Ashuru, ingawa akupiga kwa fimbo, na kuliinua gongo lake juu yako, kama walivyofanya Wamisri.
Na watu watano wa kwenu watawafukuza watu mia moja, na watu mia moja wa kwenu watawafukuza watu elfu kumi; na adui zenu wataanguka mbele yenu kwa upanga.
Utokapo kwenda vitani kupigana na adui zako, na kuona farasi, na magari, na watu wengi kuliko wewe, usiwaogope; kwa kuwa BWANA Mungu wako, yu pamoja nawe, aliyekukweza kutoka nchi ya Misri.
BWANA akamwambia Yoshua, Wewe usiogope kwa ajili ya hao; kwani kesho wakati kama huu nitawatoa wakiwa wameuawa wote mbele ya Israeli; utawakata farasi wao, na magari yao utayateketeza kwa moto.