Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wafalme 17:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

8 Wakaziendea sheria za mataifa, ambao BWANA aliwafukuza mbele ya wana wa Israeli, na sheria za wafalme wa Israeli walizozifanya.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 na kufuata njia za mataifa ambayo Mwenyezi-Mungu aliyafukuza mbele ya Waisraeli, na kufanya matendo ya wafalme wa Israeli waliyoyaingiza nchini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 na kufuata njia za mataifa ambayo Mwenyezi-Mungu aliyafukuza mbele ya Waisraeli, na kufanya matendo ya wafalme wa Israeli waliyoyaingiza nchini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 na kufuata njia za mataifa ambayo Mwenyezi-Mungu aliyafukuza mbele ya Waisraeli, na kufanya matendo ya wafalme wa Israeli waliyoyaingiza nchini.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 na kufuata desturi za mataifa ambayo Mwenyezi Mungu alikuwa ameyafukuza mbele yao, pamoja na desturi ambazo wafalme wa Israeli walizileta.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 na kufuata desturi za mataifa ambayo bwana alikuwa ameyafukuza mbele yao, pamoja na desturi ambazo wafalme wa Israeli walizileta.

Tazama sura Nakili




2 Wafalme 17:8
19 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa hiyo mfalme akafanya shauri, akatengeneza ng'ombe wawili wa dhahabu, akawaambia watu, Ni vigumu kwenu kupanda kwenda Yerusalemu; tazama, hii ndiyo miungu yenu, enyi Israeli, iliyowapandisha kutoka nchi ya Misri.


Akachukiza mno, kwa kuzifuata sanamu sawasawa na yote waliyoyafanya Waamori, BWANA aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.)


Naye mfalme Ahazi akaenda Dameski ili aonane na Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akaiona ile madhabahu iliyokuwako Dameski. Mfalme Ahazi akamletea Uria kuhani namna yake ile madhabahu, na cheo chake, kama ilivyokuwa kazi yake yote.


Lakini aliiendea njia ya wafalme wa Israeli, hata akampitisha mwanawe motoni, sawasawa na machukizo ya mataifa BWANA aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.


Hata na watu wa Yuda hawakuyashika maagizo ya BWANA, Mungu wao, lakini walikwenda katika amri za Israeli walizokuwa wamezifanya wenyewe.


Walakini hawakusikia, bali wakafanya sawasawa na kawaida zao za kwanza.


Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, sawasawa na machukizo ya mataifa, aliowafukuza BWANA mbele ya wana wa Israeli.


Bali walijichanganya na mataifa, Wakajifunza matendo yao.


Usiisujudie miungu yao, wala kuitumikia; wala usitende mfano wa matendo yao; bali utaiangamiza kabisa, na nguzo zao utazivunja vipande vipande.


BWANA asema hivi, Msijifunze njia ya mataifa, wala msishangae kwa sababu ya ishara za mbinguni; maana mataifa hushangaa kwa sababu ya ishara hizo.


Nao umeasi amri zangu, kwa kutenda mabaya kuliko mataifa hayo, nao umeasi sheria kuliko nchi hizo ziuzungukazo; maana wamezikataa hukumu zangu, wala hawakuenda katika sheria zangu.


Efraimu ameonewa, amesetwa katika hukumu, kwa sababu alikuwa radhi kufuata ubatili.


Nanyi msifanye matendo kama yale ya nchi ya Misri mlikokaa; wala msifanye matendo kama yale ya nchi ya Kanaani, nitakayowapeleka; wala msifuate amri zao hao.


Msifanye sanamu yoyote, wala msijisimamishie sanamu ya kuchonga, wala mnara, wala msiweke jiwe lolote lililochorwa katika nchi yenu ili kulisujudia; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.


Kwa maana amri za Omri ndizo zishikwazo, na matendo yote ya nyumba ya Ahabu, nanyi mnakwenda katika mashauri yao; ili nikufanye kuwa ukiwa, na wenyeji waliomo humo kuwa zomeo; nanyi mtayachukua matukano waliyotukanwa watu wangu.


Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo