Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Wafalme 16:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Mfalme Ahazi akakata papi za vitako, akaliondoa lile birika juu yake; akaiteremsha ile bahari itoke juu ya ng'ombe za shaba zilizokuwa chini yake, akaiweka juu ya sakafu ya mawe.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Mfalme Ahazi aliziondoa papi zilizokuwa zimesimamishwa huko, akaondoa birika lililoitwa bahari ambalo lilikuwa juu ya wale fahali kumi na wawili wa shaba na kuliweka juu ya msingi wa mawe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Mfalme Ahazi aliziondoa papi zilizokuwa zimesimamishwa huko, akaondoa birika lililoitwa bahari ambalo lilikuwa juu ya wale fahali kumi na wawili wa shaba na kuliweka juu ya msingi wa mawe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Mfalme Ahazi aliziondoa papi zilizokuwa zimesimamishwa huko, akaondoa birika lililoitwa bahari ambalo lilikuwa juu ya wale fahali kumi na wawili wa shaba na kuliweka juu ya msingi wa mawe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Mfalme Ahazi akaondoa mbao za pembeni na kuondoa masinia kwenye vile vishikilio vilivyohamishika. Akaondoa ile Bahari kutoka mafahali wa shaba walioishikilia, na kuiweka kwenye kitako cha jiwe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Mfalme Ahazi akaondoa mbao za pembeni na kuondoa masinia kwenye vile vishikilio vilivyohamishika. Akaondoa ile Bahari kutoka kwenye mafahali wa shaba walioishikilia, na kuiweka kwenye kitako cha jiwe.

Tazama sura Nakili

2 Wafalme 16:17
8 Marejeleo ya Msalaba  

Akafanya hivyo Uria kuhani, sawasawa na yote aliyoyaamuru mfalme Ahazi.

Na ukumbi wa sabato walioujenga katika hiyo nyumba, na mahali pa kuingia pake mfalme palipokuwapo nje, akavigeuza kuikabili nyumba ya BWANA, kwa sababu ya mfalme wa Ashuru.

Tena Ahazi akakusanya vyombo vyote vya nyumba ya Mungu, akavikata vipande vipande vyombo vya nyumba ya Mungu, akaifunga milango ya nyumba ya BWANA; akajijengea madhabahu katika kila pembe ya Yerusalemu.

Tena vyombo vyote alivyovitupa mfalme Ahazi alipotawala, hapo alipoasi, tumevitengeza na kuvitakasa; navyo, tazama, vipo mbele ya madhabahu ya BWANA.

Nguzo mbili, beseni, na ng'ombe kumi na mbili za shaba zilizokuwa chini ya vikalio vyake, ambavyo mfalme Sulemani aliifanyia nyumba ya BWANA; shaba ya vitu hivyo vyote ilikuwa haiwezi kupimwa kwa kuwa nyingi sana.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo