Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Wafalme 15:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Na Shalumu mwana wa Yabeshi akafanya fitina juu yake, akampiga mbele ya watu, akamwua, akatawala mahali pake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Shalumu mwana wa Yabeshi alikula njama dhidi ya mfalme Zekaria, akampiga mbele ya watu na kumwua, kisha akatawala mahali pake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Shalumu mwana wa Yabeshi alikula njama dhidi ya mfalme Zekaria, akampiga mbele ya watu na kumwua, kisha akatawala mahali pake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Shalumu mwana wa Yabeshi alikula njama dhidi ya mfalme Zekaria, akampiga mbele ya watu na kumwua, kisha akatawala mahali pake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Shalumu mwana wa Yabeshi akapanga njama dhidi ya Zekaria. Akamshambulia mbele ya watu, akamuua, na akawa mfalme baada yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Shalumu mwana wa Yabeshi akafanya shauri baya dhidi ya Zekaria. Akamshambulia mbele ya watu, akamuua na kuingia mahali pake kuwa mfalme.

Tazama sura Nakili




2 Wafalme 15:10
16 Marejeleo ya Msalaba  

Mwaka wa tatu wa Asa mfalme wa Yuda Baasha akamwua, akatawala mahali pake.


Kwa maana Yozakari mwana wa Shimeathi, na Yehozabadi mwana wa Shomeri, watumishi wake, wakampiga, naye akafa; wakamzika pamoja na babaze mjini mwa Daudi. Na Amazia mwanawe akatawala mahali pake.


Wakafanya fitina juu yake katika Yerusalemu, naye akakimbia mpaka Lakishi, lakini wakatuma watu kumfuata mpaka Lakishi, wakamwua huko.


Basi mambo yote ya Zekaria yaliyosalia, tazama, yameandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Israeli.


Menahemu mwana wa Gadi akapanda kutoka Tirza, akaja Samaria, akampiga Shalumu mwana wa Yabeshi huko Samaria, akamwua, akatawala mahali pake.


Menahemu akalala na babaze; na Pekahia mwanawe akatawala mahali pake.


Na Peka mwana wa Remalia, jemadari wake, akamfanyia uhaini, akampiga huko Samaria, katika ngome ya nyumba ya mfalme, pamoja na Argobu na Arie; na pamoja naye walikuwako watu hamsini wa Wagileadi. Akamwua, akatawala mahali pake.


Na Hoshea mwana wa Ela akamfitinia Peka mwana wa Remalia, akampiga, akamwua, akatawala mahali pake, katika mwaka wa ishirini wa Yothamu mwana wa Uzia.


Akafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA kama walivyofanya babaze; hakuyaacha makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli.


Yehu akavuta upinde wake kwa nguvu zake zote, akampiga Yoramu kati ya mikono yake, hata mshale ukamtoka penye moyo wake, akaanguka katika gari lake.


Hata Yehu alipoingia lango la mji, alisema, Je! Ni amani, Ewe Zimri, mwenye kumwua bwana wako?


Wote wamepata moto kama tanuri, nao hula watawala wao; wafalme wao wote wameanguka; hakuna hata mmoja wao aniitaye mimi.


Wamesimamisha wafalme, lakini si kwa shauri langu; wamejifanyia wakuu, lakini nilikuwa sina habari; kwa fedha yao na dhahabu yao wamejifanyia sanamu, kusudi wakatiliwe mbali.


na mahali palipoinuka pa Isaka patakuwa ukiwa, na mahali patakatifu pa Israeli pataharibika; nami nitaondoka nishindane na nyumba ya Yeroboamu kwa upanga.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo