Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wafalme 13:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

20 Elisha akafa, nao wakamzika. Basi vikosi vya Wamoabi wakaingia katika nchi mwanzo wa mwaka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Elisha alifariki, akazikwa. Kila mwaka, makundi ya Wamoabu yalikuja kuishambulia nchi ya watu wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Elisha alifariki, akazikwa. Kila mwaka, makundi ya Wamoabu yalikuja kuishambulia nchi ya watu wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Elisha alifariki, akazikwa. Kila mwaka, makundi ya Wamoabu yalikuja kuishambulia nchi ya watu wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Al-Yasa akafa, nao wakamzika. Vikosi vya Wamoabu vilikuwa vinashambulia nchi kwa vita kila mwaka wakati wa vuli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Al-Yasa akafa, nao wakamzika. Vikosi vya Wamoabu vilikuwa vinashambulia nchi kwa vita kila mwaka wakati wa vuli.

Tazama sura Nakili




2 Wafalme 13:20
13 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa, baada ya mambo hayo, Yusufu akaambiwa, Tazama, baba yako ni mgonjwa; akawatwaa wanawe wawili, Manase na Efraimu, pamoja naye.


Basi Yakobo alipokwisha kuwaagiza wanawe, akakunja miguu yake kitandani, akafa, akakusanywa pamoja na watu wake.


Naye BWANA akatuma juu yake vikosi vya Wakaldayo, na vikosi vya Washami, na vikosi vya Wamoabi, na vikosi vya wana wa Amoni, akawatuma juu ya Yuda ili kuiharibu, sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa mkono wa watumishi wake manabii.


Lakini ikawa, Ahabu alipokufa, mfalme wa Moabu akamwasi mfalme wa Israeli.


Akaenda akatuma kwa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akasema, Mfalme wa Moabu ameniasi; je! Utakwenda pamoja nami tupigane na Moabu? Akasema, Nitakwenda; mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, farasi wangu ni kama farasi wako.


Na Washami walikuwa wametoka vikosi, wakachukua mfungwa mmoja kijana mwanamke kutoka nchi ya Israeli; naye akamhudumia mkewe Naamani.


Basi akawaandalia chakula tele; nao walipokwisha kula na kunywa, akawaacha, wakaenda zao kwa bwana wao. Na vikosi vya Shamu havikuja tena katika nchi ya Israeli.


Wakamzika katika mji wa Daudi kati ya wafalme, kwa sababu ametenda mema katika Israeli, na kwa Mungu, na katika nyumba yake.


Je, Baba zenu wako wapi? Je, manabii nao wanaishi milele?


Watu watauwa wakamzika Stefano, wakamfanyia maombolezo makuu.


Basi wana wa Israeli walifanya yaliyo maovu tena mbele za BWANA; naye BWANA akamtia nguvu Egloni mfalme wa Moabu juu ya Israeli, kwa sababu walikuwa wameyafanya yaliyo maovu mbele za macho ya BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo