Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wafalme 12:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

16 Lakini fedha ya matoleo ya kosa, na fedha ya matoleo ya dhambi, haikuletwa nyumbani mwa BWANA; hiyo ilikuwa ya makuhani wenyewe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Fedha zilizotolewa kuwa sadaka za hatia na sadaka za kuondoa dhambi hazikuingizwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu; hizo zilikuwa ni mali ya makuhani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Fedha zilizotolewa kuwa sadaka za hatia na sadaka za kuondoa dhambi hazikuingizwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu; hizo zilikuwa ni mali ya makuhani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Fedha zilizotolewa kuwa sadaka za hatia na sadaka za kuondoa dhambi hazikuingizwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu; hizo zilikuwa ni mali ya makuhani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Fedha zilizopatikana kutokana na sadaka za hatia na sadaka za dhambi hazikuletwa katika Hekalu la Mwenyezi Mungu; zilikuwa mali ya makuhani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Fedha zilizopatikana kutokana na sadaka za hatia na sadaka za dhambi hazikuletwa katika Hekalu la bwana; zilikuwa mali ya makuhani.

Tazama sura Nakili




2 Wafalme 12:16
9 Marejeleo ya Msalaba  

Nami nikawaweka watunza hazina juu ya hazina, yaani, Shelemia kuhani, na Sadoki mwandishi, na wa Walawi, Pedaya; na wa pili wao alikuwa Hanani, mwana wa Zakuri, mwana wa Matania; kwani walihesabiwa kuwa waaminifu, na ilikuwa juu yao kuwagawia ndugu zao.


Hujilisha dhambi ya watu wangu, hujifurahisha moyo kwa uovu wao.


kisha ataweka mkono wake kichwani mwake huyo mbuzi, na kumchinja hapo wachinjapo sadaka ya kuteketezwa mbele za BWANA; ni sadaka ya dhambi.


Naye ataweka mkono wake kichwani mwake hiyo sadaka ya dhambi, na kumchinja sadaka ya dhambi mahali hapo pa sadaka ya kuteketezwa.


Kama hiyo sadaka ya dhambi ilivyo, na sadaka ya hatia ni vivyo hivyo; sheria yake ni moja; huyo kuhani afanyaye upatanisho kwayo, ndiye atakayekuwa nayo.


Sadaka zote za kuinuliwa za vitu vitakatifu, wana wa Israeli wavisongezavyo kwa BWANA, nimekupa wewe na wanao na binti zako pamoja nawe, ni haki yenu ya milele; ni agano la chumvi la milele mbele za BWANA kwa ajili yako, na kizazi chako pamoja nawe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo