Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Samueli 22:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

20 Akanitoa akanipeleka panapo nafasi; Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Alinileta, akaniweka mahali pa usalama, alinisalimisha, kwani alipendezwa nami.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Alinileta, akaniweka mahali pa usalama, alinisalimisha, kwani alipendezwa nami.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Alinileta, akaniweka mahali pa usalama, alinisalimisha, kwani alipendezwa nami.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Alinileta nje mahali penye nafasi tele, akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Alinileta nje mahali penye nafasi tele, akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami.

Tazama sura Nakili




2 Samueli 22:20
16 Marejeleo ya Msalaba  

Akaondoka huko akachimba kisima kingine, wala hicho hawakukigombania. Akakiita jina lake Rehobothi, akasema, Kwa kuwa sasa BWANA ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi.


lakini akisema kama hivi, Mimi si radhi nawe kabisa; basi, mimi hapa, na anitendee kama aonavyo kuwa vyema.


Umezifanyia nafasi hatua zangu, Wala miguu yangu haikuteleza.


Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibariki kweli kweli, na kuipanua mipaka yangu, na mkono wako ukawa pamoja nami, nawe ungenilinda nisipatwe na maovu wala madhara! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.


Katika shida yangu nilimwita BWANA; BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi.


BWANA huwaridhia wao wamchao, Na kuzitarajia fadhili zake.


Kwa kuwa BWANA awaridhia watu wake, Huwapamba wenye upole kwa wokovu.


Husema, Umtegemee BWANA; na amponye; Na amwokoe sasa, maana apendezwa naye.


Wala hukunitia mikononi mwa adui; Miguu yangu umeisimamisha mahali penye usalama.


Ee BWANA, unifadhili, maana ni katika dhiki, Jicho langu limenyauka kwa masumbufu, Naam, mwili wangu na nafsi yangu.


Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu.


Kwa maana Israeli ametenda kwa ukaidi, kama ndama mkaidi; sasa je! BWANA atawalisha kama mwana-kondoo katika mahali penye malisho mazuri.


Alipokuwa bado akisema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye.


Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kama anamtaka; kwa maana alisema, Mimi ni Mwana wa Mungu.


na tazama, sauti kutoka mbinguni ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo