Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 9:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 Na malkia wa Sheba aliposikia sifa za Sulemani, alikuja ili amjaribu Sulemani kwa maswali ya fumbo huko Yerusalemu, akiwa na wafuasi wengi, na ngamia wachukuao manukato, na dhahabu nyingi sana, na vito vya thamani; alipomfikia Sulemani, akamwambia mambo yote aliyokuwa nayo moyoni mwake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Malkia wa Sheba aliposikia sifa za Solomoni, aliwasili Yerusalemu ili kumjaribu Solomoni kwa maswali magumu. Alifuatana na msafara wa watu, pamoja na ngamia waliobeba manukato, dhahabu nyingi sana na vito vya thamani. Na alipofika kwa Solomoni, alimwuliza maswali yote aliyokuwa nayo moyoni mwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Malkia wa Sheba aliposikia sifa za Solomoni, aliwasili Yerusalemu ili kumjaribu Solomoni kwa maswali magumu. Alifuatana na msafara wa watu, pamoja na ngamia waliobeba manukato, dhahabu nyingi sana na vito vya thamani. Na alipofika kwa Solomoni, alimwuliza maswali yote aliyokuwa nayo moyoni mwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Malkia wa Sheba aliposikia sifa za Solomoni, aliwasili Yerusalemu ili kumjaribu Solomoni kwa maswali magumu. Alifuatana na msafara wa watu, pamoja na ngamia waliobeba manukato, dhahabu nyingi sana na vito vya thamani. Na alipofika kwa Solomoni, alimwuliza maswali yote aliyokuwa nayo moyoni mwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Malkia wa Sheba aliposikia habari za umaarufu wa Sulemani, akaja Yerusalemu kumjaribu kwa maswali magumu. Alifika akiwa na msafara mkubwa sana, wenye ngamia waliobeba vikolezo, dhahabu nyingi, na vito vya thamani. Alikuja kwa Sulemani na kuzungumza naye mambo yote aliyokuwa nayo moyoni mwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Malkia wa Sheba aliposikia habari za umaarufu wa Sulemani, huyo malkia akaja Yerusalemu kumjaribu kwa maswali magumu. Alifika akiwa na msafara mkubwa sana, pamoja na ngamia waliobeba vikolezi, kiasi kikubwa cha dhahabu na vito vya thamani, alikuja kwa Sulemani na kuzungumza naye kuhusu yote ambayo alikuwa nayo moyoni mwake.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 9:1
23 Marejeleo ya Msalaba  

na Obali, na Abimaeli, na Seba,


Na wana wa Kushi ni Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama ni Sheba, na Dedani.


Yokshani akamzaa Sheba, na Dedani; na wana wa Dedani walikuwa Waashuri na Waletushi, na Waleumi.


Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; kuliko Ethani Mwezrahi, na Hemani, na Kalkoli, na Darda, wana wa Maholi; zikaenea sifa zake kati ya mataifa yote yaliyozunguka.


Basi Sulemani, mwana wa Daudi, alijiimarisha katika ufalme wake, naye BWANA, Mungu wake, alikuwa pamoja naye, akamtukuza mno.


basi hekima na maarifa umepewa; nami nitakupa mali, na utajiri, na utukufu, kupita walivyokuwa navyo wafalme wote waliokuwa kabla yako, wala baada yako hapatakuwa na mtu atakayekuwa navyo.


Naye Sulemani akamfumbulia maswali yake yote; wala halikuwako neno alilofichiwa Sulemani, asimwambie.


Basi akampa mfalme talanta mia moja na ishirini za dhahabu, na manukato mengi mengi sana, na vito vya thamani; wala hapakuwapo manukato mengi kama hayo aliyopewa mfalme Sulemani na malkia wa Sheba.


Nitafunua mbele zake malalamiko yangu, Shida yangu nitaitangaza mbele zake.


Nitatega sikio langu nisikie mithali, Na kufumbua fumbo langu kwa kinubi.


Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete kodi; Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa.


Na aishi maisha marefu! Na wampe dhahabu ya Sheba; Na wamwombee daima; Na kumbariki mchana kutwa.


Nitafumbua kinywa changu kwa mithali, Niyatamke mafumbo ya kale.


Kufahamu mithali na kitendawili, na maneno ya wenye hekima na mafumbo yao.


Wingi wa ngamia utakufunika, Ngamia vijana wa Midiani na Efa; Wote watakuja kutoka Sheba; Wataleta dhahabu na uvumba; Na kuzitangaza sifa za BWANA.


Enyi wazawa wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.


Malkia wa kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho za dunia ili asikie hekima ya Sulemani, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.


Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa.


ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema, Nitafumbua kinywa changu kwa mifano, Nitayatamka yaliyositirika tangu kuumbwa kwa ulimwengu.


Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu, uvumba na manemane.


Malkia wa Kusini ataondoka siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa na hatia; kwa sababu yeye alikuja kutoka ncha za dunia aisikie hekima ya Sulemani; na hapa pana mkubwa kuliko Sulemani.


Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni, mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho yangu mbele za BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo