Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 7:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

2 Wala makuhani hawakuweza kuingia nyumbani mwa BWANA, kwa kuwa utukufu wa BWANA umeijaza nyumba ya BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Kwa kuwa utukufu wa Mwenyezi-Mungu ulijaa nyumba ya Mwenyezi-Mungu, makuhani hawakuweza kuingia humo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Kwa kuwa utukufu wa Mwenyezi-Mungu ulijaa nyumba ya Mwenyezi-Mungu, makuhani hawakuweza kuingia humo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Kwa kuwa utukufu wa Mwenyezi-Mungu ulijaa nyumba ya Mwenyezi-Mungu, makuhani hawakuweza kuingia humo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Makuhani hawakuweza kuingia ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu kwa sababu utukufu wa Mwenyezi Mungu ulilijaza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Makuhani hawakuweza kuingia ndani ya Hekalu la bwana kwa sababu utukufu wa bwana ulilijaza.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 7:2
7 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa, makuhani walipotoka katika patakatifu, nyumba ya BWANA ikajaa wingu;


hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru BWANA nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu BWANA, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya BWANA,


hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya lile wingu; kwa kuwa nyumba ya Mungu imejaa utukufu wa BWANA.


BWANA, nimependa makao ya nyumba yako, Na mahali pa maskani ya utukufu wako.


Na kuonekana kwake ule utukufu wa BWANA kulikuwa kama moto uteketezao, juu ya mlima machoni pa wana wa Israeli.


Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA wa majeshi.


Hekalu likajazwa moshi uliotoka kwenye utukufu wa Mungu na uweza wake. Wala hapakuwa na mtu aliyeweza kuingia ndani ya hekalu, mpaka yatimizwe mapigo saba ya wale malaika saba.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo