Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 5:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Wakaja wazee wote wa Israeli, nao Walawi wakajitwika sanduku.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Baada ya wazee wote wa Israeli kuwasili, Walawi walilibeba sanduku la agano,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Baada ya wazee wote wa Israeli kuwasili, Walawi walilibeba sanduku la agano,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Baada ya wazee wote wa Israeli kuwasili, Walawi walilibeba sanduku la agano,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Wazee wote wa Israeli walipofika, Walawi wakajitwika Sanduku la Agano,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Wazee wote wa Israeli walipofika, Walawi wakajitwika Sanduku la Agano,

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 5:4
8 Marejeleo ya Msalaba  

Wazee wote wa Israeli wakaja, nao makuhani wakajitwika sanduku.


Ndipo Daudi akasema, Haimpasi mtu awaye yote kulichukua sanduku la Mungu, isipokuwa Walawi peke yao; kwa kuwa hao ndio aliowachagua BWANA, ili walichukue sanduku la Mungu, na kumtumikia daima.


Wakalipandisha sanduku, na ile hema ya kukutania, na vyombo vitakatifu vyote vilivyokuwamo Hemani, vitu hivyo makuhani Walawi wakavipandisha.


Makuhani wakaliingiza sanduku la Agano la BWANA mahali pake katika chumba cha ndani cha nyumba, patakatifu pa patakatifu, yaani, chini ya mabawa ya makerubi.


Na Haruni na wanawe watakapokwisha kupafunika mahali patakatifu, na vyombo vyote vya mahali patakatifu, hapo watakapong'oa kambi; baadaye, wana wa Kohathi watakuja kuvichukua; lakini wasiviguse vile vitu vitakatifu, wasife. Vyombo vile ni mzigo wa wana wa Kohathi katika hema ya kukutania.


Kisha Yoshua akawaambia makuhani, akasema, Liinueni sanduku la Agano, mkavuke mbele ya hao watu. Wakaliinua sanduku la Agano, wakatangulia mbele ya watu.


Bali Yoshua, mwana wa Nuni, akawaita makuhani, akawaambia, Lichukueni sanduku la Agano, tena makuhani saba na wachukue mabaragumu saba za pembe za kondoo dume watangulie mbele ya sanduku la BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo