Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 36:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

20 Na wale waliookoka na upanga akawachukua mpaka Babeli; wakamtumikia yeye na wanawe hata kulipoingia milki ya Uajemi;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Watu walionusurika vitani aliwachukua uhamishoni Babuloni. Huko wakawa watumwa wake na wa wazawa wake mpaka mwanzo wa ufalme wa Persia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Watu walionusurika vitani aliwachukua uhamishoni Babuloni. Huko wakawa watumwa wake na wa wazawa wake mpaka mwanzo wa ufalme wa Persia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Watu walionusurika vitani aliwachukua uhamishoni Babuloni. Huko wakawa watumwa wake na wa wazawa wake mpaka mwanzo wa ufalme wa Persia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Wale watu walionusurika kuuawa kwa upanga wakachukuliwa kwenda uhamishoni Babeli. Nao wakawa watumishi wake na wa wanawe hadi wakati wa utawala wa ufalme wa Uajemi ulifika.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Wale watu walionusurika kuuawa kwa upanga wakachukuliwa kwenda uhamishoni Babeli. Nao wakawa watumishi wake na wa wanawe mpaka wakati wa utawala wa ufalme wa Uajemi ulifika.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 36:20
13 Marejeleo ya Msalaba  

Na mabaki ya watu waliosalia katika mji, nao wale walioasi, na kumkimbilia mfalme wa Babeli, na mabaki ya watu wote wengine, watu hao Nebuzaradani, kamanda wa askari walinzi, akawachukua mateka.


Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la BWANA alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, BWANA akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema,


Basi hawa ndio watu wa mkoa, waliokwea kutoka katika ule uhamisho wa hao waliokuwa wamechukuliwa, ambao Nebukadneza, mfalme wa Babeli, aliwachukua mateka mpaka Babeli, nao wakarudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake;


Lakini hapo baba zetu walipomkasirisha Mungu wa mbingu na nchi, hata akaghadhibika, akawatia katika mkono wa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, Mkaldayo, naye ndiye aliyeiharibu nyumba hii, akawachukua watu mateka mpaka Babeli.


Nilikuwa nimekasirika na watu wangu, niliutia unajisi urithi wangu, nikawatia mkononi mwako; wewe hukuwatendea rehema; kwa wazee uliifanya nira yako kuwa nzito sana.


Na nchi hii yote pia itakuwa ukiwa, na kitu cha kushangaza; nayo mataifa haya yatamtumikia mfalme wa Babeli miaka sabini.


Na mataifa yote watamtumikia yeye, na mwanawe, na mwana wa mwanawe, hata utakapowadia wakati wa nchi yake mwenyewe, ndipo mataifa mengi na wafalme wakuu watamtumikisha yeye.


Watu hawa ndio wale ambao Nebukadneza aliwachukua mateka; katika mwaka wa saba, Wayahudi elfu tatu na ishirini na watatu;


Na sasa umepandwa jangwani, katika nchi kavu, ya ukame.


Uajemi, na Kushi, na Putu, pamoja nao; wote wana ngao na chapeo;


Uwe na uchungu, utaabike ili uzae, Ee binti Sayuni, kama mwanamke mwenye uchungu; maana sasa utatoka mjini, nawe utakaa katika mashamba; utafika hata Babeli; huko ndiko utakakookolewa; huko ndiko BWANA atakakokukomboa kutoka kwa mikono ya adui zako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo