2 Mambo ya Nyakati 35:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC7 Tena Yosia akawapa watu, matoleo ya makundi, wana-kondoo na wana-mbuzi, yote yawe kwa ajili ya matoleo ya Pasaka, wote waliokuwako, wakiwa elfu thelathini, na ng'ombe elfu tatu; hao walitoka katika mali za mfalme. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema7 Kisha Yosia aliwapa watu, wanambuzi wapatao 30,000, na mafahali 3,000, wote hawa walitolewa kwenye mifugo ya mfalme. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND7 Kisha Yosia aliwapa watu, wanambuzi wapatao 30,000, na mafahali 3,000, wote hawa walitolewa kwenye mifugo ya mfalme. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza7 Kisha Yosia aliwapa watu, wanambuzi wapatao 30,000, na mafahali 3,000, wote hawa walitolewa kwenye mifugo ya mfalme. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu7 Ndipo Yosia akawapa watu wote waliokuwepo wana-mbuzi na kondoo wapatao elfu thelathini kwa ajili ya sadaka ya Pasaka, pia na ng’ombe elfu kumi; wote kutoka kwa mali binafsi ya mfalme. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu7 Ndipo Yosia akawapa watu wote wana-mbuzi waliokuwepo jumla ya kondoo wapatao 30,000 kwa ajili ya sadaka ya Pasaka, pia na ng’ombe 10,000, vyote hivi kutoka mali binafsi ya mfalme. Tazama sura |
Tena itakuwa kazi ya mkuu kutoa hizo sadaka za kuteketezwa, na sadaka za unga, na sadaka za vinywaji, katika sikukuu, na katika mwezi mpya, na katika sabato, katika sikukuu zote za nyumba ya Israeli zilizoamriwa; atatengeneza sadaka ya dhambi, na sadaka ya unga, na sadaka ya kuteketezwa, na sadaka za amani, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nyumba ya Israeli.