Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 35:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

6 Mkachinje Pasaka, mkajitakase, mkawatengenezee ndugu zenu, kutenda sawasawa na neno la BWANA kwa mkono wa Musa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Mchinjeni mwanakondoo wa Pasaka, mjitakase, halafu itayarisheni kwa ajili ya ndugu zenu, ili waweze kutimiza agizo la Mwenyezi-Mungu lililosemwa na Mose.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Mchinjeni mwanakondoo wa Pasaka, mjitakase, halafu itayarisheni kwa ajili ya ndugu zenu, ili waweze kutimiza agizo la Mwenyezi-Mungu lililosemwa na Mose.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Mchinjeni mwanakondoo wa Pasaka, mjitakase, halafu itayarisheni kwa ajili ya ndugu zenu, ili waweze kutimiza agizo la Mwenyezi-Mungu lililosemwa na Mose.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Chinjeni mwana-kondoo wa Pasaka, jitakaseni, nanyi kwa niaba ya koo zenu fanyeni maandalizi, mkitenda sawasawa na neno la Mwenyezi Mungu kwa mkono wa Musa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Chinjeni mwana-kondoo wa Pasaka, jitakaseni, nanyi kwa niaba ya koo zenu fanyeni maandalizi, mkitenda sawasawa na neno la bwana kwa mkono wa Musa.”

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 35:6
21 Marejeleo ya Msalaba  

Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake, na wote waliokuwa pamoja naye, Ondoeni miungu migeni iliyoko kwenu, mjisafishe mkabadili nguo zenu.


akawaambia, Ninyi ni vichwa vya koo za baba za Walawi; jitakaseni, ninyi na ndugu zenu, ili mlipandishe sanduku la BWANA, Mungu wa Israeli, mpaka mahali pale nilipolitayarishia.


Wakawakusanya ndugu zao, wakajitakasa, wakaingia, kama alivyoamuru mfalme kwa maneno ya BWANA, ili waisafishe nyumba ya BWANA.


Lakini makuhani walikuwa wachache, wasiweze kuchuna sadaka zote za kuteketezwa; basi ndugu zao Walawi wakawasaidia, hadi kazi ilipokwisha na hadi makuhani walipojitakasa; kwa kuwa Walawi walikuwa wenye mioyo ya adili kwa kujitakasa kuliko makuhani.


akawaambia, Nisikieni, enyi Walawi; jitakaseni nafsi zenu sasa, mkaitakase na nyumba ya BWANA, Mungu wa baba zenu, mkautoe uchafu katika patakatifu.


Kwa sababu hawakuweza kuifanya wakati ule, kwa kuwa makuhani wa kutosha walikuwa hawajajitakasa, wala watu hawajakusanyika huko Yerusalemu.


Naye Yosia akamfanyia BWANA Pasaka huko Yerusalemu; wakachinja Pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.


Wakachinja Pasaka, nao makuhani wakamimina damu waliyopokea mikononi mwao, Walawi wakachuna.


Tena Yosia akawapa watu, matoleo ya makundi, wana-kondoo na wana-mbuzi, yote yawe kwa ajili ya matoleo ya Pasaka, wote waliokuwako, wakiwa elfu thelathini, na ng'ombe elfu tatu; hao walitoka katika mali za mfalme.


Ikawa makuhani walipokwisha kutoka katika patakatifu; (kwani makuhani wote waliokuwapo, walikuwa wamejitakasa, wala hawakuzishika zamu zao;


Basi ilikuwa, hapo hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao akawatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kusongeza sadaka za kuteketezwa kama hesabu yao wote ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Pengine hawa wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Ndivyo alivyofanya Ayubu sikuzote.


Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.


Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule; na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni.


BWANA akamwambia Musa, Nenda kwa watu hawa, ukawatakase leo na kesho, wakazifue nguo zao,


Akawaambia watu; Muwe tayari siku ya tatu; msimkaribie mwanamke.


Kusanyeni watu, litakaseni kusanyiko, Kusanyeni wazee, kusanyeni watoto, Na hao wanyonyao maziwa; Bwana arusi na atoke chumbani mwake, Na bibi arusi katika hema yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo