Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 35:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

2 Akawaweka makuhani katika kazi zao, akawatia moyo kutumika katika nyumba ya BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Aliwateua makuhani kwa kazi zao ambazo walihitajika kufanya katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu na kuwatia moyo wazifanye kikamilifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Aliwateua makuhani kwa kazi zao ambazo walihitajika kufanya katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu na kuwatia moyo wazifanye kikamilifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Aliwateua makuhani kwa kazi zao ambazo walihitajika kufanya katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu na kuwatia moyo wazifanye kikamilifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Akawaweka makuhani kwenye wajibu wao na kuwatia moyo katika utumishi wa Hekalu la Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Akawaweka makuhani kwenye wajibu wao na kuwatia moyo katika utumishi wa Hekalu la bwana.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 35:2
9 Marejeleo ya Msalaba  

Basi sasa jitieni moyo na nia kumtafuta BWANA, Mungu wenu; inukeni basi, mkamjengee BWANA Mungu mahali patakatifu, ili kulileta sanduku la Agano la BWANA, na vyombo vitakatifu vya Mungu, ndani ya nyumba itakayojengwa kwa ajili ya jina la BWANA.


Yehoyada akauamuru usimamizi wa nyumba ya BWANA chini ya mkono wa makuhani Walawi, aliowagawa Daudi nyumbani mwa BWANA, ili wazisongeze sadaka za kuteketezwa za BWANA, kama ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, kwa kufurahi na kuimba, kama alivyoamuru Daudi.


Basi Walawi na Yuda wote wakafanya kama alivyowaamuru Yehoyada kuhani; wakawatwaa kila mtu watu wake, hao watakaoingia siku ya sabato, na wale watakaotoka siku ya sabato; kwa maana Yehoyada kuhani hakuwaruhusu waondoke.


Hezekia akaziweka zamu za makuhani na Walawi kwa zamu zao, kila mtu kwa kadiri ya huduma yake, makuhani na Walawi pia, kwa sadaka za kuteketezwa na kwa sadaka za amani, kutumika, na kushukuru, na kusifu, malangoni mwa kambi ya BWANA.


Wakawaweka makuhani katika sehemu zao, wakawaweka na Walawi katika zamu zao, kwa ajili ya huduma ya Mungu, iliyokuwako Yerusalemu; kama ilivyoandikwa katika chuo cha Musa.


Dada yake mtoto akasimama mbali ili ajue yatakayompata.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo