Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 35:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Wakachinja Pasaka, nao makuhani wakamimina damu waliyopokea mikononi mwao, Walawi wakachuna.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Walimchinja mwanakondoo wa Pasaka, nao makuhani walinyunyiza damu, waliyopokea kutoka kwao nao Walawi waliwachuna wanyama.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Walimchinja mwanakondoo wa Pasaka, nao makuhani walinyunyiza damu, waliyopokea kutoka kwao nao Walawi waliwachuna wanyama.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Walimchinja mwanakondoo wa Pasaka, nao makuhani walinyunyiza damu, waliyopokea kutoka kwao nao Walawi waliwachuna wanyama.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Wana-kondoo wa Pasaka wakachinjwa, nao makuhani wakanyunyiza ile damu waliyokabidhiwa, wakati Walawi wakiwa wanawachuna wale wanyama ngozi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Wana-kondoo wa Pasaka wakachinjwa, nao makuhani wakanyunyiza ile damu waliyokabidhiwa, wakati Walawi wakiwa wanawachuna wale wanyama ngozi.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 35:11
11 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini makuhani walikuwa wachache, wasiweze kuchuna sadaka zote za kuteketezwa; basi ndugu zao Walawi wakawasaidia, hadi kazi ilipokwisha na hadi makuhani walipojitakasa; kwa kuwa Walawi walikuwa wenye mioyo ya adili kwa kujitakasa kuliko makuhani.


Wakasimama mahali pao kwa taratibu yao, kulingana na Torati ya Musa, mtu wa Mungu; nao makuhani wakainyunyiza damu, waliyoipokea mikononi mwa Walawi.


Naye Yosia akamfanyia BWANA Pasaka huko Yerusalemu; wakachinja Pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.


Wakaziondoa sadaka za kuteketezwa, wawape watu kama makundi yalivyo kwa kufuata nyumba za nasaba zao, ili wamtolee BWANA, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Musa. Nao ng'ombe wakawafanya vivyo hivyo.


Mkachinje Pasaka, mkajitakase, mkawatengenezee ndugu zenu, kutenda sawasawa na neno la BWANA kwa mkono wa Musa.


Kwa maana makuhani na Walawi walikuwa wamejitakasa wote pamoja; wote walikuwa hali ya tohara; wakachinja Pasaka kwa ajili ya wana wote wa uhamisho, na kwa ajili ya ndugu zao makuhani, na kwa ajili ya nafsi zao.


Nao watahudumu kwa kufuata amri yako, na kuhudumu hemani pote; lakini wasikaribie vyombo vya patakatifu, wala madhabahu, wasife, wao pamoja na ninyi.


Nawe na wanao pamoja nawe mtautunza ukuhani wenu, kwa ajili ya kila kitu cha madhabahu, na kwa ajili ya vile vilivyomo ndani ya pazia, nanyi mtatumika. Nawapeni ukuhani kuwa utumishi wa kipawa; na mgeni akaribiaye atauawa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo