Basi mtu huyo akapiga kelele juu ya madhabahu, kwa neno la BWANA akasema, Ee madhabahu, madhabahu, BWANA asema hivi, Angalia, mtoto atazaliwa katika nyumba ya Daudi, jina lake Yosia; na juu yako atawatambika makuhani wa mahali pa juu, wanaofukiza uvumba juu yako, na mifupa ya watu itateketezwa juu yako.
Naye Yosia alipogeuka, aliyaona makaburi yale yaliyokuwako huko, juu ya mlima; akatuma watu, akaitoa ile mifupa katika yale makaburi, akaiteketeza juu ya madhabahu, akainajisi, sawasawa na lile neno la BWANA, alilolinena yule mtu wa Mungu, aliyetamka mambo hayo.
Naye Yosia akayaondolea mbali machukizo yote katika nchi zote zilizokuwa milki ya wana wa Israeli, akawafanya wote walioonekana katika Israeli kutumika, naam, wamtumikie BWANA, Mungu wao. Siku zake zote hawakuacha kumfuata BWANA, Mungu wa baba zao.
Akazibomoa madhabahu, akazipondaponda Maashera na sanamu kuwa mavumbi, akazikatakata sanamu zote za jua katika nchi yote ya Israeli, kisha akarejea Yerusalemu.
Hivi hamtaitia unajisi nchi ambayo mwakaa; kwa kuwa damu huitia nchi unajisi; wala hapana sadaka itoshayo kwa ajili ya nchi, kwa ajili ya damu iliyomwagwa ndani yake, isipokuwa ni damu ya huyo aliyeimwaga.