Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Mambo ya Nyakati 34:33 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

33 Naye Yosia akayaondolea mbali machukizo yote katika nchi zote zilizokuwa milki ya wana wa Israeli, akawafanya wote walioonekana katika Israeli kutumika, naam, wamtumikie BWANA, Mungu wao. Siku zake zote hawakuacha kumfuata BWANA, Mungu wa baba zao.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

33 Kisha Yosia aliondoa sanamu zote za kuchukiza zilizokuwa katika eneo lote la watu wa Israeli, na kuwahimiza watu wote wa Israeli kumtumikia Mwenyezi-Mungu, Mungu wao. Katika maisha yake yote hawakumwacha Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

33 Kisha Yosia aliondoa sanamu zote za kuchukiza zilizokuwa katika eneo lote la watu wa Israeli, na kuwahimiza watu wote wa Israeli kumtumikia Mwenyezi-Mungu, Mungu wao. Katika maisha yake yote hawakumwacha Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

33 Kisha Yosia aliondoa sanamu zote za kuchukiza zilizokuwa katika eneo lote la watu wa Israeli, na kuwahimiza watu wote wa Israeli kumtumikia Mwenyezi-Mungu, Mungu wao. Katika maisha yake yote hawakumwacha Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

33 Yosia akaondoa machukizo yote ya sanamu kutoka nchi yote ya Waisraeli na akawataka wale wote waliokuwa katika Israeli wamtumikie Mwenyezi Mungu, Mungu wao. Kwa muda wote alioishi, hawakushindwa kumfuata Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

33 Yosia akaondoa machukizo yote ya sanamu kutoka nchi yote iliyokuwa mali ya Waisraeli na akawataka wale wote waliokuwako katika Israeli wamtumikie bwana Mwenyezi Mungu wao. Kwa muda wote alioishi, hawakushindwa kumfuata bwana, Mungu wa baba zao.

Tazama sura Nakili

2 Mambo ya Nyakati 34:33
9 Marejeleo ya Msalaba  

Akawafanya wote walioonekana katika Yerusalemu na Benyamini walikubali. Na wenyeji wa Yerusalemu wakafanya kulingana na agano la Mungu, Mungu wa baba zao.

Maana nimezishika njia za BWANA, Wala sikumwasi Mungu wangu.

Na pamoja na hayo yote dada yake, Yuda mwenye hiana, hajanirudia mimi kwa moyo wake wote, bali kwa unafiki, asema BWANA.

Kama ukitaka kurudi, Ee Israeli, asema BWANA, utanirudia mimi; na kama ukitaka kuyaondoa machukizo yako, yasiwe mbele ya macho yangu, ndipo hutaondolewa;

Ee Efraimu, nikutendee nini? Ee Yuda, nikutendee nini? Kwa maana fadhili zenu ni kama wingu la asubuhi na kama umande utowekao mapema.

Nao Israeli wakamtumikia BWANA siku zote za Yoshua, na siku zote za hao wazee walioishi baada ya kufa kwake Yoshua, hao walioijua kazi yote ya BWANA, aliyowatendea Israeli.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo