Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Mambo ya Nyakati 34:30 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

30 Akapanda mfalme nyumbani kwa BWANA, na watu wote wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu, na makuhani na Walawi, na watu wote, wakubwa kwa wadogo; naye akasoma masikioni mwao maneno yote ya Kitabu cha Agano kilichoonekana nyumbani mwa BWANA.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Naye mfalme akaenda katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu pamoja na wanaume wote wa Yuda, na wakazi wa Yerusalemu wakifuatana na makuhani, Walawi na watu wengine wote wakubwa kwa wadogo. Ndipo alipowasomea maneno ya kitabu cha agano kilichopatikana katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Naye mfalme akaenda katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu pamoja na wanaume wote wa Yuda, na wakazi wa Yerusalemu wakifuatana na makuhani, Walawi na watu wengine wote wakubwa kwa wadogo. Ndipo alipowasomea maneno ya kitabu cha agano kilichopatikana katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 Akapanda kwenda hekaluni mwa Mwenyezi Mungu pamoja na watu wa Yuda, watu wa Yerusalemu, makuhani na Walawi, watu wote, wakubwa kwa wadogo. Akasoma wakiwa wanasikia maneno yote ya Kitabu cha Agano, kilichokuwa kimepatikana katika Hekalu la Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 Akapanda kwenda hekaluni mwa bwana pamoja na watu wa Yuda, watu wa Yerusalemu, makuhani na Walawi, watu wote, wakubwa kwa wadogo. Akasoma wakiwa wanasikia maneno yote ya Kitabu cha Agano, ambacho kilikuwa kimepatikana katika Hekalu la bwana.

Tazama sura Nakili

2 Mambo ya Nyakati 34:30
19 Marejeleo ya Msalaba  

Mfalme akapanda kwenda nyumbani kwa BWANA, na watu wote wa Yuda, nao wote waliokaa Yerusalemu, pamoja naye, na makuhani, na manabii, na watu wote, wadogo kwa wakubwa; akasoma masikioni mwao maneno yote ya Kitabu cha Agano kilichoonekana katika nyumba ya BWANA.

Naye mfalme akawaamuru watu wote, akasema, Mfanyieni BWANA, Mungu wenu, Pasaka, kama ilivyoandikwa katika kitabu hiki cha agano.

Basi mfalme wa Shamu alikuwa amewaamuru makamanda wa magari yake, akisema, Msipigane na mdogo wala mkuu, ila na mfalme wa Israeli peke yake.

Akajibu Hilkia akamwambia Shafani mwandishi, Kitabu cha Torati nimekiona nyumbani mwa BWANA. Hilkia akampa Shafani kile kitabu.

BWANA asema hivi, Angalia, nitaleta mabaya juu ya mahali hapa, na juu ya wakazi wake, laana zote zilizoandikwa katika kitabu hicho walichokisoma mbele ya mfalme wa Yuda;

Akasimama mfalme mahali pake, akafanya agano mbele za BWANA, kumfuata BWANA, na kuzishika amri zake, na shuhuda zake, na sheria zake, kwa moyo wake wote, na kwa roho yake yote, kuyatenda maneno ya agano yaliyoandikwa kitabuni humo.

Wakuu na wadogo wako huko; Mtumishi yuko huru kwa bwana wake.

Kisha akakitwaa Kitabu cha Agano akakisoma masikioni mwa watu; wakasema, Hayo yote aliyoyanena BWANA tutayatenda, nasi tutatii.

Mimi, Mhubiri, nilikuwa Mfalme wa Israeli katika Yerusalemu.

Naye mkuu atakapoingia, ataingia katikati yao, nao, watakapotoka, watatoka wote pamoja.

Msitazame nafsi za watu katika hukumu; muwasikize wadogo na wakubwa sawasawa; msiche uso wa mtu yeyote; kwa kuwa hukumu ni ya Mungu; na lile neno liwashindalo mniletee mimi, nami nitalisikiza.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo