Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 34:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

26 Lakini kwa mfalme wa Yuda, aliyewatuma kumwuliza BWANA, mtamwambia hivi, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi; Kuhusu uliyoyasikia,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Lakini kumhusu mfalme wa Yuda, aliyewatuma kutafuta shauri la Mwenyezi-Mungu mwambie kwamba, hivi ndivyo anavyosema Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli juu ya maneno uliyoyasikia:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Lakini kumhusu mfalme wa Yuda, aliyewatuma kutafuta shauri la Mwenyezi-Mungu mwambie kwamba, hivi ndivyo anavyosema Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli juu ya maneno uliyoyasikia:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Lakini kumhusu mfalme wa Yuda, aliyewatuma kutafuta shauri la Mwenyezi-Mungu mwambie kwamba, hivi ndivyo anavyosema Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli juu ya maneno uliyoyasikia:

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Mwambieni mfalme wa Yuda, ambaye amewatuma kumuuliza Mwenyezi Mungu, ‘Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, kuhusu maneno uliyoyasikia:

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Mwambieni mfalme wa Yuda, ambaye amewatuma kumuuliza bwana, ‘Hivi ndivyo asemavyo bwana, Mungu wa Israeli kuhusu maneno uliyoyasikia:

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 34:26
5 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini yule mfalme wa Yuda, aliyewatuma ninyi kumwuliza BWANA, mtamwambia hivi, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa habari ya maneno yale uliyoyasikia,


Nendeni, mkamwulize BWANA kwa ajili yangu, na kwa hao waliosalia wa Israeli na wa Yuda, kuhusu habari za maneno ya kitabu kilichoonekana; maana ghadhabu ya BWANA ni nyingi iliyomwagika juu yetu, kwa sababu baba zetu hawakulishika neno la BWANA, kutenda sawasawa na yote yaliyoandikwa kitabuni humo.


Akawaambia, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi; Mwambieni mtu huyo aliyewatuma kwangu,


kwa sababu wameniacha mimi, na kuifukizia uvumba miungu mingine, ili wanikasirishe mimi kwa matendo yote ya mikono yao; kwa hiyo ghadhabu yangu imemwagika juu ya mahali hapa, wala isizimike.


kwa kuwa moyo wako ulikuwa mwororo, nawe umejinyenyekeza mbele ya Mungu, uliposikia maneno yake juu ya mahali hapa, na juu ya wakazi wake, ukajinyenyekeza mbele zangu, na kuyararua mavazi yako, na kulia mbele zangu; mimi nami nimekusikia, asema BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo