Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 34:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 Nao walipotoa ile fedha iliyoletwa nyumbani mwa BWANA, Hilkia kuhani akakiona kitabu cha Torati ya BWANA iliyotolewa kwa mkono wa Musa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Wakati walipokuwa wanashughulika na utoaji wa fedha zilizokuwa zimeletwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, kuhani Hilkia alipata Kitabu cha Sheria ya Mwenyezi-Mungu iliyotolewa kwa mkono wa Mose.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Wakati walipokuwa wanashughulika na utoaji wa fedha zilizokuwa zimeletwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, kuhani Hilkia alipata Kitabu cha Sheria ya Mwenyezi-Mungu iliyotolewa kwa mkono wa Mose.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Wakati walipokuwa wanashughulika na utoaji wa fedha zilizokuwa zimeletwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, kuhani Hilkia alipata Kitabu cha Sheria ya Mwenyezi-Mungu iliyotolewa kwa mkono wa Mose.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Wakati walikuwa wakizitoa nje fedha zilizokuwa zimetolewa kwenye Hekalu la Mwenyezi Mungu, kuhani Hilkia akakipata kile Kitabu cha Torati ya Mwenyezi Mungu kilichokuwa kimetolewa kwa mkono wa Musa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Wakati walikuwa wakizitoa nje fedha zilizokuwa zimetolewa kwenye Hekalu la bwana, kuhani Hilkia akakipata kile Kitabu cha Torati ya bwana kilichokua kimetolewa kwa mkono wa Musa.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 34:14
19 Marejeleo ya Msalaba  

Na walipokwisha kumwita mfalme, wakatokewa na Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna, mwandishi, na Yoa, mwana wa Asafu, mwenye kuandika tarehe.


Ikawa ulipothibitika ufalme wa Rehoboamu, naye amepata nguvu, aliiacha Torati ya BWANA, na Israeli wote pamoja naye.


Tena akawaamuru watu waliokaa Yerusalemu, watoe sehemu ya makuhani na Walawi, ili hao wajibidiishe katika Torati ya BWANA.


Akajibu Hilkia akamwambia Shafani mwandishi, Kitabu cha Torati nimekiona nyumbani mwa BWANA. Hilkia akampa Shafani kile kitabu.


Wakamjia Hilkia kuhani mkuu, wakampa fedha, iliyoletwa nyumbani mwa Mungu, waliyoikusanya Walawi, mabawabu, mikononi mwa Manase na Efraimu, na mabaki yote ya Israeli, na Yuda yote na Benyamini, na wenyeji wa Yerusalemu.


Basi mambo yote ya Yosia yaliyosalia, na matendo yake mema, sawasawa na yote yaliyoandikwa katika Torati ya BWANA,


Kwa maana huyo Ezra alikuwa ameuelekeza moyo wake kuitafuta sheria ya BWANA, na kuitenda, na kufundisha maagizo na hukumu katika Israeli.


Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.


Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya BWANA;


Kwa hiyo kama vile muali wa moto uteketezavyo mabua makavu, na kama manyasi makavu yaangukavyo katika muali wa moto; kadhalika shina lao litakuwa kama ubovu, na ua lao litapeperushwa juu kama mavumbi; kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA wa majeshi, na kulidharau neno lake aliye Mtakatifu wa Israeli.


Mwasemaje, Sisi tuna akili, na Torati ya BWANA tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.


tena mpate kuwafundisha wana wa Israeli amri hizi zote ambazo BWANA amewaambia kwa mkono wa Musa.


Hizi ni amri, maagizo na sheria, BWANA alizozifanya kati ya yeye na hao wana wa Israeli katika huo mlima wa Sinai kwa mkono wa Musa.


Basi Haruni na wanawe wakafanya mambo hayo yote BWANA aliyoyaagiza kwa mkono wa Musa.


Basi, walipokwisha kuyatimiza yote kama yalivyoagizwa katika sheria ya Bwana, walirejea Galilaya mpaka mjini kwao, Nazareti.


Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda kulingana na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo