Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 33:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

20 Basi Manase akalala na babaze, wakamzika nyumbani mwake; na Amoni mwanawe akatawala mahali pake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Manase alifariki na kuzikwa katika ikulu yake, naye Amoni, mwanawe, akatawala mahali pake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Manase alifariki na kuzikwa katika ikulu yake, naye Amoni, mwanawe, akatawala mahali pake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Manase alifariki na kuzikwa katika ikulu yake, naye Amoni, mwanawe, akatawala mahali pake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Manase akalala na baba zake, akazikwa katika jumba lake la kifalme. Naye Amoni mwanawe akawa mfalme baada yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Manase akalala pamoja na baba zake akazikwa katika jumba lake la kifalme. Naye Amoni mwanawe akawa mfalme baada yake.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 33:20
9 Marejeleo ya Msalaba  

na mwanawe huyo ni Amoni; na mwanawe huyo ni Yosia.


Alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipoanza kutawala, akatawala huko Yerusalemu miaka minane; akafariki bila kutamaniwa; wakamzika mjini mwa Daudi, ila si katika makaburi ya wafalme.


Hezekia akalala na babaze, wakamzika mahali pa kupandia makaburi ya wana wa Daudi; nao Yuda wote na wenyeji wa Yerusalemu wakamfanyia heshima alipokufa. Na Manase mwanawe akatawala mahali pake.


Sala yake pia, na jinsi Mungu alivyomtakabali, na dhambi yake yote, na kosa lake, na mahali alipopajenga mahali pa juu, na kupasimamishia Maashera na sanamu za kuchonga, kabla ya kujinyenyekeza; tazama, hayo yameandikwa katika Kumbukumbu ya Hozai.


Amoni alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka miwili.


Neno la BWANA lililomjia Sefania, mwana wa Kushi, mwana wa Gedalia, mwana wa Amaria, mwana wa Hezekia; katika siku za Yosia, mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda.


Hezekia akamzaa Manase; Manase akamzaa Amoni; Amoni akamzaa Yosia;


Akafa Samweli; nao Israeli wote wakakusanyika, wakamwomboleza, wakamzika nyumbani mwake huko Rama. Kisha Daudi akaondoka, akashuka mpaka nyikani mwa Maoni.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo