Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 32:31 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

31 Lakini kuhusu wajumbe wa wakuu wa Babeli, waliotumwa kwake kuuliza ajabu iliyofanywa katika nchi, Mungu akamwacha, ili amjaribu, ili kwamba ayajue yote yaliyokuwamo moyoni mwake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

31 na hata wakati ambapo mabalozi wa wakuu wa Babuloni waliotumwa kwake kuuliza juu ya mambo ya ajabu yaliyotokea humo, Mungu, alimwacha ajiamulie mwenyewe, ili amjaribu na kujua yote yaliyokuwa moyoni mwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

31 na hata wakati ambapo mabalozi wa wakuu wa Babuloni waliotumwa kwake kuuliza juu ya mambo ya ajabu yaliyotokea humo, Mungu, alimwacha ajiamulie mwenyewe, ili amjaribu na kujua yote yaliyokuwa moyoni mwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

31 na hata wakati ambapo mabalozi wa wakuu wa Babuloni waliotumwa kwake kuuliza juu ya mambo ya ajabu yaliyotokea humo, Mungu, alimwacha ajiamulie mwenyewe, ili amjaribu na kujua yote yaliyokuwa moyoni mwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

31 Lakini wajumbe walipotumwa na watawala wa Babeli kumuuliza kuhusu ishara ambayo ilifanyika nchini, Mungu alimwacha ili kumjaribu na kujua kila kitu kilichokuwa moyoni mwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

31 Lakini wakati wajumbe walipotumwa na watawala wa Babeli kumuuliza juu ya ishara ambayo ilitokea katika nchi, Mungu alimwacha ili kumjaribu na kujua kila kitu kilichokuwa moyoni mwake.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 32:31
24 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Abrahamu, akamwambia, Ee Abrahamu! Naye akasema, Mimi hapa.


Katika siku hizo Hezekia akaugua akawa katika hatari ya kufa; akamwomba BWANA; naye akasema naye, akampa ishara.


Walakini Hezekia hakuwa na shukrani kadiri alivyofadhiliwa; kwa kuwa moyo wake ulijawa na kiburi; kwa hiyo ikawako hasira juu yake, na juu ya Yuda na Yerusalemu.


Basi mambo yote ya Hezekia yaliyosalia, na matendo yake mema, tazama, yameandikwa katika maono ya nabii Isaya, mwana wa Amozi, katika Kitabu cha Wafalme wa Yuda na Israeli.


Usinifiche uso wako, Usimkatalie mtumishi wako kwa hasira. Umekuwa msaada wangu, usinitupe, Wala usiniache, Ee Mungu wa wokovu wangu.


Kalibu ni kwa fedha, na tanuri kwa dhahabu; Bali BWANA huijaribu mioyo.


Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina langu, nami nitawasikia; mimi nitasema, Watu hawa ndio wangu; nao watasema, BWANA ndiye Mungu wangu.


Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamuwezi kufanya neno lolote.


wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda BWANA, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote.


aliyekulisha jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zako; apate kukutweza, apate kukujaribu, ili kukutendea mema mwisho wako.


Nawe utaikumbuka njia ile yote BWANA, Mungu wako aliyokuongoza miaka hii arubaini katika jangwa, ili akunyenyekeze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo.


Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.


ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.


Kisha akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema, Nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa BWANA amemwacha.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo