Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 32:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

3 akafanya shauri na wakuu wake, na wakuu wa majeshi yake, kuzuia maji ya chemchemi zilizokuwa nje ya mji; nao wakamsaidia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 aliamua, yeye pamoja na maofisa wake wakuu wa majeshi kuyafunga maji ya chemchemi zilizokuwa nje ya miji; nao wakamuunga mkono, wakamsaidia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 aliamua, yeye pamoja na maofisa wake wakuu wa majeshi kuyafunga maji ya chemchemi zilizokuwa nje ya miji; nao wakamuunga mkono, wakamsaidia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 aliamua, yeye pamoja na maofisa wake wakuu wa majeshi kuyafunga maji ya chemchemi zilizokuwa nje ya miji; nao wakamuunga mkono, wakamsaidia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 akafanya shauri na maafisa wake na mashujaa wake juu ya kuzuia maji kutoka chemchemi zilizo nje ya mji, nao wakamsaidia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 akafanya shauri na maafisa wake na mashujaa wake juu ya kuzuia maji kutoka chemchemi zilizo nje ya mji, nao wakamsaidia.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 32:3
13 Marejeleo ya Msalaba  

Wewe wasema, lakini ni maneno yasiyo na maana, kwamba, Lipo shauri na zipo nguvu kwa vita hivi. Basi, unamtumaini nani hata ukaniasi mimi?


Basi mambo yote ya Hezekia yaliyosalia, na ushujaa wake wote, tena alivyolifanya birika na mfereji, akaleta maji ndani ya mji, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Yuda?


Kwa maana mfalme na wakuu wake, na kusanyiko lote katika Yerusalemu walikubaliana kuiadhimisha Pasaka mwezi wa pili.


Basi Hezekia, alipoona ya kuwa Senakeribu amekuja, na kuazimia kupigana na Yerusalemu,


Naye huyo Hezekia ndiye aliyezuia chemchemi ya juu ya maji ya Gihoni, akayaleta chini moja kwa moja upande wa magharibi wa mji wa Daudi. Akafanikiwa Hezekia katika kazi zake zote.


Wakakusanyika watu wengi, wakazizuia chemchemi zote, na kijito kilichopita kati ya nchi, wakisema, Kwa nini, wakifika wafalme wa Ashuru, waone maji mengi?


Pasipo ushauri mipango vuhunjika; Bali kwa wingi wa washauri huthibitika.


Kila kusudi huthibitika kwa kushauriana; Na kwa shauri la akili fanya vita.


Maana kwa mashauri ya akili utafanya vita; Na kwa wingi wa washauri huja wokovu.


Ni nani aliyemwongoza Roho ya BWANA, na kumfundisha kwa kuwa mshauri wake?


Teka maji yawe tayari kwa kuzingirwa kwako; Zitie nguvu ngome zako; Ingia katika udongo, yakanyage matope, Itie nguvu tanuri ya kuokea matofali.


Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo