Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 32:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

29 Tena akajitengenezea miji, na mali za kondoo na ng'ombe kwa wingi; maana Mungu alimtajirisha sana sana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Vivyo hivyo alijiongezea miji kwa ajili yake mwenyewe, makundi mengi ya ng'ombe na kondoo kwa sababu Mwenyezi-Mungu alimkirimia mali nyingi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Vivyo hivyo alijiongezea miji kwa ajili yake mwenyewe, makundi mengi ya ng'ombe na kondoo kwa sababu Mwenyezi-Mungu alimkirimia mali nyingi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Vivyo hivyo alijiongezea miji kwa ajili yake mwenyewe, makundi mengi ya ng'ombe na kondoo kwa sababu Mwenyezi-Mungu alimkirimia mali nyingi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Akajenga vijiji na kujipatia idadi kubwa ya kondoo na mbuzi, pamoja na ng’ombe, kwa kuwa Mungu alikuwa amempa utajiri mwingi sana.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Akajenga vijiji na kujipatia idadi kubwa ya kondoo na mbuzi, pamoja na ng’ombe kwa kuwa Mungu alikuwa amempa utajiri mwingi sana.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 32:29
15 Marejeleo ya Msalaba  

Utajiri na heshima hutoka kwako wewe, nawe watawala juu ya vyote; na mkononi mwako mna uweza na nguvu; tena mkononi mwako mna kuwatukuza na kuwawezesha wote.


Akafa akiwa mzee sana, mwenye maisha marefu, mali na heshima; naye Sulemani mwanawe akatawala badala yake.


Kwa hiyo BWANA akauthibitisha ufalme mkononi mwake; Yehoshafati akaletewa zawadi na watu wote wa Yuda; basi akawa na mali na heshima tele.


Amazia akamwambia mtu wa Mungu, Lakini tuzifanyieje zile talanta mia moja nilizowapa jeshi la Israeli? Mtu wa Mungu akajibu, BWANA aweza kukupa zaidi sana kuliko hizo.


Akajenga minara tena nyikani, akachimba mabwawa mengi, maana alikuwa na ng'ombe tele; katika Shefela pia, na katika nchi tambarare; tena alikuwa na wakulima na watunza mizabibu milimani, na katika mashamba ya neema; maana yeye alipenda ukulima.


ghala pia za mazao ya nafaka na mvinyo na mafuta; na malisho ya mifugo ya namna zote, na makundi mazizini.


Mali yake nayo ilikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watumishi wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki.


Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Je! Huyo Ayubu anamcha BWANA bure?


Basi hivyo BWANA akaubariki huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake; naye alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na jozi za ng'ombe elfu moja, na punda wake elfu moja.


Baraka ya BWANA hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo.


Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.


BWANA hufukarisha mtu, na hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo