Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 32:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

22 Ndivyo BWANA alivyomwokoa Hezekia, na wenyeji wa Yerusalemu kutoka mkono wa Senakeribu, mfalme wa Ashuru, na mikononi mwa wote, akawaongoza pande zote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Kwa njia hii basi, Mwenyezi-Mungu akamwokoa mfalme Hezekia na wakazi wa Yerusalemu kutoka mkono wa Senakeribu mfalme wa Ashuru, na kutoka mkono wa maadui wake wote. Akawapa maisha ya amani na jirani zake wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Kwa njia hii basi, Mwenyezi-Mungu akamwokoa mfalme Hezekia na wakazi wa Yerusalemu kutoka mkono wa Senakeribu mfalme wa Ashuru, na kutoka mkono wa maadui wake wote. Akawapa maisha ya amani na jirani zake wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Kwa njia hii basi, Mwenyezi-Mungu akamwokoa mfalme Hezekia na wakazi wa Yerusalemu kutoka mkono wa Senakeribu mfalme wa Ashuru, na kutoka mkono wa maadui wake wote. Akawapa maisha ya amani na jirani zake wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Hivyo Mwenyezi Mungu akamwokoa Hezekia na watu wa Yerusalemu kutoka mkononi mwa Senakeribu mfalme wa Ashuru na kutoka mikononi mwa wengine wote. Mwenyezi Mungu akawapa amani pande zote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Hivyo bwana akamwokoa Hezekia na watu wa Yerusalemu kutoka mkononi mwa Senakeribu mfalme wa Ashuru na kutoka mikononi mwa wengine wote. bwana akawastarehesha kila upande.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 32:22
16 Marejeleo ya Msalaba  

Na mabaki yaliyookoka ya nyumba ya Yuda yatatia mizizi chini, na kuzaa matunda juu.


Naye BWANA akatuma malaika aliyewakatia mbali wapiganaji vita wote, na majemadari, na makamanda, kambini mwa mfalme wa Ashuru. Basi akarudia nchi yake kwa aibu. Naye alipoingia nyumbani mwa mungu wake, baadhi ya wanawe mwenyewe wakamwangamiza humo kwa upanga.


Awapaye wafalme wokovu, Amwokoa Daudi, mtumishi wake, na upanga wa uovu.


Kwa maana ndivyo alivyo MUNGU, Mungu wetu. Milele na milele Yeye ndiye atakayetuongoza.


Utaniongoza kwa shauri lako, Na baadaye utanikaribisha kwa utukufu.


Kwa maana BWANA ndiye mwamuzi wetu; BWANA ndiye mfanya sheria wetu; BWANA ndiye mfalme wetu; ndiye atakayetuokoa.


Naye BWANA atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.


Lakini nitairehemu nyumba ya Yuda; nitawaokoa kwa BWANA, Mungu wao; wala sitawaokoa kwa upinde, wala kwa upanga, wala kwa silaha, wala kwa farasi, wala kwa wapanda farasi.


Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.


Bwana awaongoze mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na subira ya Kristo.


Hivyo BWANA akawaokoa Israeli siku ile; na vita ilienea mpaka kupita Beth-aveni, na watu wote waliokuwa pamoja na Sauli walikuwa kama wanaume elfu kumi. Vita ikanenea katika nchi yenye milima milima ya Efraimu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo