Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Mambo ya Nyakati 31:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

6 Nao wana wa Israeli na Yuda, waliokaa mijini mwa Yuda, wakaleta pia zaka za ng'ombe na kondoo, na zaka za vitu vilivyowekwa wakfu, alivyowekewa BWANA, Mungu wao, wakaviweka katika mafungu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Watu wa Israeli na Yuda walioishi katika miji ya Yuda, pia wakaleta zaka zao za ng'ombe na kondoo na vitu vingine, wakaviweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu. Waliviweka vitu hivyo katika mafungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Watu wa Israeli na Yuda walioishi katika miji ya Yuda, pia wakaleta zaka zao za ng'ombe na kondoo na vitu vingine, wakaviweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu. Waliviweka vitu hivyo katika mafungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Watu wa Israeli na Yuda walioishi katika miji ya Yuda, pia wakaleta zaka zao za ng'ombe na kondoo na vitu vingine, wakaviweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu. Waliviweka vitu hivyo katika mafungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Watu wa Israeli na Yuda walioishi katika miji ya Yuda wakaleta pia fungu la kumi la makundi yao ya ng’ombe na makundi ya kondoo na mbuzi pia na fungu la kumi la vitu vitakatifu vilivyowekwa wakfu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mungu wao, na kuvikusanya katika malundo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Watu wa Israeli na Yuda walioishi katika miji ya Yuda wakaleta pia fungu la kumi la makundi yao ya ng’ombe na makundi ya kondoo na mbuzi pia na fungu la kumi la vitu vitakatifu vilivyowekwa wakfu kwa ajili ya bwana Mwenyezi Mungu wao na kuvikusanya katika malundo.

Tazama sura Nakili

2 Mambo ya Nyakati 31:6
5 Marejeleo ya Msalaba  

Katika mwezi wa tatu wakaanza kupanga mafungu hayo, wakayamaliza katika mwezi wa saba.

nao wakasema na Musa, na kumwambia, Watu waleta vitu vingi sana zaidi ya hivyo vitoshavyo kwa ajili ya utumishi wa hiyo kazi, ambayo BWANA aliagiza ifanywe.

Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya BWANA; ni takatifu kwa BWANA.

Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la mavuno yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo