2 Mambo ya Nyakati 31:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC10 Azaria kuhani mkuu, wa nyumba ya Sadoki, akamjibu, akasema, Tangu watu walipoanza kuleta matoleo nyumbani kwa BWANA, tumekula na kushiba, na kusaza tele; kwa kuwa BWANA amewabariki watu wake; na kilichosalia ndiyo akiba hii kubwa. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema10 Azaria, kuhani mkuu aliyekuwa wa uzao wa Sadoki akamjibu, “Tangu watu waanze kuleta matoleo yao hekaluni, tumekuwa na vyakula vya kutosha na hata tunayo akiba kubwa. Mwenyezi-Mungu amewabariki watu wake, ndiyo maana tumepata vitu hivi vyote.” Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND10 Azaria, kuhani mkuu aliyekuwa wa uzao wa Sadoki akamjibu, “Tangu watu waanze kuleta matoleo yao hekaluni, tumekuwa na vyakula vya kutosha na hata tunayo akiba kubwa. Mwenyezi-Mungu amewabariki watu wake, ndiyo maana tumepata vitu hivi vyote.” Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza10 Azaria, kuhani mkuu aliyekuwa wa uzao wa Sadoki akamjibu, “Tangu watu waanze kuleta matoleo yao hekaluni, tumekuwa na vyakula vya kutosha na hata tunayo akiba kubwa. Mwenyezi-Mungu amewabariki watu wake, ndiyo maana tumepata vitu hivi vyote.” Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu10 naye Azaria aliyekuwa kuhani mkuu, kutoka jamaa ya Sadoki, akajibu, “Tangu watu walipoanza kuleta sadaka zao katika Hekalu la Mwenyezi Mungu tumekuwa na chakula cha kutosha na vingi vya kuweka akiba kwa sababu Mwenyezi Mungu amewabariki watu wake, hivyo tumekuwa na kiasi kingi kilichobaki.” Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu10 naye Azaria aliyekuwa kuhani mkuu, kutoka jamaa ya Sadoki, akajibu, “Tangu watu walipoanza kuleta sadaka zao katika Hekalu la bwana tumekuwa na chakula cha kutosha na vingi vya kuweka akiba kwa sababu bwana amewabariki watu wake, hivyo tumekuwa na kiasi kingi kilichobaki.” Tazama sura |