Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 30:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

24 Maana Hezekia, mfalme wa Yuda, aliwatolea kusanyiko matoleo ya ng'ombe elfu moja, na kondoo elfu saba; na wakuu wakawatolea kusanyiko ng'ombe elfu moja, na kondoo elfu kumi; tena wakajitakasa makuhani wengi sana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Mfalme Hezekia wa Yuda aliwapa watu waliokusanyika jumla ya mafahali 1,000 na kondoo 7,000. Hali kadhalika, wakuu wakawapa mafahali 1,000 na kondoo 10,000. Idadi kubwa ya makuhani walijitakasa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Mfalme Hezekia wa Yuda aliwapa watu waliokusanyika jumla ya mafahali 1,000 na kondoo 7,000. Hali kadhalika, wakuu wakawapa mafahali 1,000 na kondoo 10,000. Idadi kubwa ya makuhani walijitakasa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Mfalme Hezekia wa Yuda aliwapa watu waliokusanyika jumla ya mafahali 1,000 na kondoo 7,000. Hali kadhalika, wakuu wakawapa mafahali 1,000 na kondoo 10,000. Idadi kubwa ya makuhani walijitakasa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Hezekia, mfalme wa Yuda akatoa mafahali elfu moja, kondoo na mbuzi elfu saba kwa ajili ya kusanyiko, nao maafisa wakatoa mafahali elfu moja, pamoja na kondoo na mbuzi elfu kumi. Idadi kubwa ya makuhani wakajiweka wakfu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Hezekia, mfalme wa Yuda akatoa mafahali 1,000, kondoo na mbuzi 7,000 kwa ajili ya kusanyiko, nao maafisa wakatoa mafahali 1,000 pamoja na kondoo na mbuzi 10,000. Idadi kubwa ya makuhani wakajiweka wakfu.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 30:24
8 Marejeleo ya Msalaba  

Akawagawia watu wote, mkutano wote wa Israeli, wanaume kwa wanawake, kila mtu mkate wa ngano, na kipande cha nyama, na mkate wa zabibu. Basi watu wote wakaenda zao, kila mtu nyumbani kwake.


Lakini makuhani walikuwa wachache, wasiweze kuchuna sadaka zote za kuteketezwa; basi ndugu zao Walawi wakawasaidia, hadi kazi ilipokwisha na hadi makuhani walipojitakasa; kwa kuwa Walawi walikuwa wenye mioyo ya adili kwa kujitakasa kuliko makuhani.


Kisha wakaichinja Pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili, nao makuhani na Walawi wakatahayarika, wakajitakasa, wakaleta sadaka za kuteketezwa nyumbani mwa BWANA.


Kwa sababu hawakuweza kuifanya wakati ule, kwa kuwa makuhani wa kutosha walikuwa hawajajitakasa, wala watu hawajakusanyika huko Yerusalemu.


Tena itakuwa kazi ya mkuu kutoa hizo sadaka za kuteketezwa, na sadaka za unga, na sadaka za vinywaji, katika sikukuu, na katika mwezi mpya, na katika sabato, katika sikukuu zote za nyumba ya Israeli zilizoamriwa; atatengeneza sadaka ya dhambi, na sadaka ya unga, na sadaka ya kuteketezwa, na sadaka za amani, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nyumba ya Israeli.


Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo