Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 30:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

23 Na kusanyiko lote wakafanya shauri kufanya sikukuu siku saba nyingine; wakafanya sikukuu siku saba nyingine kwa furaha.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 watu waliamua kwa kauli moja kuziendeleza sherehe kwa muda wa siku saba zaidi. Basi, wakaendelea kusherehekea kwa furaha kuu kwa muda wa siku saba zaidi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 watu waliamua kwa kauli moja kuziendeleza sherehe kwa muda wa siku saba zaidi. Basi, wakaendelea kusherehekea kwa furaha kuu kwa muda wa siku saba zaidi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 watu waliamua kwa kauli moja kuziendeleza sherehe kwa muda wa siku saba zaidi. Basi, wakaendelea kusherehekea kwa furaha kuu kwa muda wa siku saba zaidi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Kisha kusanyiko lote wakakubali kuendelea na sikukuu kwa siku saba zaidi; kwa hiyo, kwa siku saba nyingine wakaendelea kuiadhimisha kwa furaha.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Kisha kusanyiko lote likakubali kuendelea na sikukuu kwa siku saba zaidi, kwa hiyo kwa siku saba nyingine wakaendelea kuiadhimisha kwa furaha.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 30:23
5 Marejeleo ya Msalaba  

Basi, wakati ule Sulemani akafanya sikukuu, na Israeli wote pamoja naye, kusanyiko kubwa sana, kutoka maingilio ya Hamathi mpaka kijito cha Misri, mbele za BWANA, Mungu wetu, siku saba na siku saba, yaani siku kumi na nne.


Tena Hezekia mfalme na wakuu wakawaamuru Walawi, wamwimbie BWANA sifa kwa maneno ya Daudi, na ya Asafu mwonaji. Wakaimba sifa kwa furaha, wakainamisha vichwa, wakaabudu.


Maana Hezekia, mfalme wa Yuda, aliwatolea kusanyiko matoleo ya ng'ombe elfu moja, na kondoo elfu saba; na wakuu wakawatolea kusanyiko ng'ombe elfu moja, na kondoo elfu kumi; tena wakajitakasa makuhani wengi sana.


Siku ya nane wakaita kusanyiko la makini; kwa maana waliadhimisha kuitakasa madhabahu siku saba, na sikukuu siku saba.


Na mkutano wote wa watu, waliorudi kutoka nchi ya uhamisho wao, wakatengeneza vibanda, wakakaa katika vibanda hivyo; maana tangu siku za Yoshua, mwana wa Nuni, hadi siku ile, wana wa Israeli hawakufanya hivyo. Pakawa na furaha kubwa sana.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo