Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 3:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Na ukumbi uliokuwa mbele yake, urefu wake ulikuwa sawa na upana wa nyumba ulikuwa dhiraa ishirini, na kimo chake mia moja na ishirini; akaufunikiza ndani kwa dhahabu safi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Chumba cha sehemu ya kuingilia kilikuwa na urefu wa mita 9, sawa na upana wa nyumba hiyo, na kimo chake mita 54. Kuta zake zilifunikwa kwa dhahabu safi upande wa ndani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Chumba cha sehemu ya kuingilia kilikuwa na urefu wa mita 9, sawa na upana wa nyumba hiyo, na kimo chake mita 54. Kuta zake zilifunikwa kwa dhahabu safi upande wa ndani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Chumba cha sehemu ya kuingilia kilikuwa na urefu wa mita 9, sawa na upana wa nyumba hiyo, na kimo chake mita 54. Kuta zake zilifunikwa kwa dhahabu safi upande wa ndani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Ukumbi wa mbele wa Hekalu ulikuwa na urefu wa dhiraa ishirini, yaani kuanzia upande mmoja hadi upande mwingine wa upana wa nyumba hiyo, na kimo chake dhiraa thelathini. Akaufunika ndani kwa dhahabu safi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Ukumbi wa mbele wa Hekalu ulikuwa na urefu wa dhiraa ishirini, yaani, kuanzia upande mmoja hadi upande mwingine wa upana wa nyumba hiyo na kimo chake dhiraa thelathini. Akaufunika ndani kwa dhahabu safi.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 3:4
6 Marejeleo ya Msalaba  

Na ukumbi mbele ya hekalu la nyumba, urefu wake ulikuwa mikono ishirini, kadiri ya upana wa nyumba; na upana wake mikono kumi mbele ya nyumba.


Basi wakaanza kutakasa siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, hata siku ya nane ya mwezi wakafika katika ukumbi wa BWANA; wakaitakasa nyumba ya BWANA katika muda wa siku nane; wakamaliza siku ya kumi na sita ya mwezi wa kwanza.


Ndipo akanileta mpaka ukumbi wa nyumba, akapima kila mwimo wa ukumbi, dhiraa tano upande huu, na dhiraa tano upande huu; na upana wa lango ulikuwa dhiraa tatu upande huu, na dhiraa tatu upande huu.


Naye Yesu alikuwa akitembea hekaluni, katika ukumbi wa Sulemani.


Basi alipokuwa akiwashika Petro na Yohana, watu wote wakawakusanyikia mbio katika tao lile lililoitwa tao la Sulemani, wakishangaa sana.


Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; nao wote walikuwako kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo