Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

2 Mambo ya Nyakati 3:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Na mabawa ya makerubi hayo urefu wake ulikuwa mikono ishirini; bawa moja mikono mitano, likiufikia ukuta wa nyumba; na bawa la pili mikono mitano, likishikana na bawa la kerubi la pili.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Kila kiumbe kilikuwa na mabawa mawili yenye urefu wa mita 4.4 jumla, mita 2.25 kila bawa. Bawa mojawapo liligusa ukuta upande mmoja wa chumba na la pili liligusana na la kiumbe wa pili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Kila kiumbe kilikuwa na mabawa mawili yenye urefu wa mita 4.4 jumla, mita 2.25 kila bawa. Bawa mojawapo liligusa ukuta upande mmoja wa chumba na la pili liligusana na la kiumbe wa pili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Kila kiumbe kilikuwa na mabawa mawili yenye urefu wa mita 4.4 jumla, mita 2.25 kila bawa. Bawa mojawapo liligusa ukuta upande mmoja wa chumba na la pili liligusana na la kiumbe wa pili.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Urefu wa mabawa ya hao makerubi ulikuwa jumla ya dhiraa ishirini. Bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa dhiraa tano, nalo liligusa ukuta wa Hekalu; bawa lake lingine lilikuwa pia na urefu wa dhiraa tano, ambalo liligusa bawa la kerubi mwingine.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Urefu wa mabawa ya hao makerubi ulikuwa jumla ya dhiraa ishirini. Bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa dhiraa tano, nalo liligusa ukuta wa Hekalu, bawa lake lingine, lilikuwa pia na urefu wa dhiraa tano, ambalo liligusa bawa la kerubi lingine.

Tazama sura Nakili

2 Mambo ya Nyakati 3:11
4 Marejeleo ya Msalaba  

Akayaweka hayo makerubi katika nyumba ya ndani; na mabawa ya makerubi yakanyoshwa, bawa la moja likafika ukutani huko, na bawa la kerubi la pili likafika ukutani huko; mabawa yao yakagusana katikati ya nyumba.

Na ndani ya nyumba ya patakatifu pa patakatifu akatengeneza makerubi mawili ya kuchonga; wakayafunika kwa dhahabu.

Na bawa la kerubi la pili lilikuwa mikono mitano, likiufikia ukuta wa nyumba; na bawa la pili mikono mitano, likishikana na bawa la kerubi la kwanza.

mabawa yao yaliungana, hili na hili; nao hawakugeuka walipokwenda, walikwenda kila mmoja kuelekea mbele.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo