Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Mambo ya Nyakati 3:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 Ndipo Sulemani akaanza kuijenga nyumba ya BWANA huko Yerusalemu, juu ya mlima Moria, pale BWANA alipomtokea Daudi babaye alipotengeza mahali pale alipoagiza Daudi, katika kiwanja cha kupuria cha Arauna Myebusi.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Kisha Solomoni alianza kujenga nyumba ya Mwenyezi-Mungu katika Yerusalemu juu ya mlima Moria ambapo Mwenyezi-Mungu alimtokea Daudi baba yake, mahali ambapo Daudi alikuwa amepachagua, kwenye kiwanja cha kupuria cha Ornani Myebusi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Kisha Solomoni alianza kujenga nyumba ya Mwenyezi-Mungu katika Yerusalemu juu ya mlima Moria ambapo Mwenyezi-Mungu alimtokea Daudi baba yake, mahali ambapo Daudi alikuwa amepachagua, kwenye kiwanja cha kupuria cha Ornani Myebusi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Kisha Solomoni alianza kujenga nyumba ya Mwenyezi-Mungu katika Yerusalemu juu ya mlima Moria ambapo Mwenyezi-Mungu alimtokea Daudi baba yake, mahali ambapo Daudi alikuwa amepachagua, kwenye kiwanja cha kupuria cha Ornani Myebusi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Ndipo Sulemani akaanza kujenga Hekalu la Mwenyezi Mungu katika Yerusalemu juu ya Mlima Moria, pale ambapo Mwenyezi Mungu alikuwa amemtokea Daudi baba yake. Ilikuwa katika kiwanja cha kupuria cha Arauna Myebusi, mahali palipotolewa na Daudi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Ndipo Sulemani akaanza kujenga Hekalu la bwana katika Yerusalemu juu ya Mlima Moria, pale ambapo bwana alikuwa amemtokea Daudi baba yake. Ilikuwa katika kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi, mahali palipotolewa na Daudi.

Tazama sura Nakili

2 Mambo ya Nyakati 3:1
10 Marejeleo ya Msalaba  

Abrahamu akapaita mahali hapo Yehova-yire, kama watu wasemavyo hata leo, Katika mlima wa BWANA itapatikana.

Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.

Lakini huyo malaika aliponyosha mkono wake kuelekea Yerusalemu ili auharibu, BWANA akaghairi katika mabaya, akamwambia huyo malaika mwenye kuwaharibu watu, Yatosha, sasa ulegeze mkono wako. Naye yule malaika wa BWANA alikuwako karibu na kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi.

Ndipo huyo malaika wa BWANA akamwamuru Gadi kwamba amwambie Daudi, ya kuwa Daudi akwee, akamwinulie BWANA madhabahu katika kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi.

Ndipo Daudi akasema, Hii ndiyo nyumba ya BWANA Mungu, na hii ndiyo madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya Israeli.

na Yohana akamzaa Azaria (ndiye huyo aliyefanya kazi ya ukuhani katika nyumba aliyoijenga Sulemani huko Yerusalemu)

Akaanza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili katika mwaka wa nne wa kutawala kwake.

Lakini Sulemani alimjengea nyumba.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo