Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 29:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

32 Na hesabu ya sadaka hizo za kuteketezwa mkutano walizozileta ni ng'ombe dume sabini, kondoo dume mia moja, na wana-kondoo mia mbili; hao wote walikuwa ni sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 Sadaka za kuteketeza walizoleta jumla zilikuwa mafahali 70, kondoo madume 100 na wanakondoo 200. Zote hizo zilikuwa sadaka za kuteketeza kwa Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 Sadaka za kuteketeza walizoleta jumla zilikuwa mafahali 70, kondoo madume 100 na wanakondoo 200. Zote hizo zilikuwa sadaka za kuteketeza kwa Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 Sadaka za kuteketeza walizoleta jumla zilikuwa mafahali 70, kondoo madume 100 na wanakondoo 200. Zote hizo zilikuwa sadaka za kuteketeza kwa Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 Idadi ya sadaka za kuteketezwa zilizoletwa na kusanyiko zilikuwa mafahali sabini, kondoo dume mia moja, na wana-kondoo dume mia mbili. Wote hawa walikuwa kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 Idadi ya sadaka za kuteketezwa zilizoletwa na kusanyiko zilikuwa mafahali sabini, kondoo dume 100 na wana-kondoo dume 200. Wote hawa walikuwa kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa bwana.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 29:32
10 Marejeleo ya Msalaba  

Basi mfalme akaenda Gibeoni, ili atoe dhabihu huko; kwa kuwa ndipo mahali pa juu palipo pakuu. Sulemani akatoa sadaka elfu moja za kuteketezwa juu ya madhabahu ile.


Sulemani akatoa sadaka za amani, alizomtolea BWANA, ng'ombe elfu ishirini na mbili, na kondoo elfu mia moja na ishirini. Ndivyo mfalme na wana wa Israeli wote walivyoiweka wakfu nyumba ya BWANA.


Siku ya pili yake, wakamtolea BWANA dhabihu, wakamchinjia BWANA sadaka ya kuteketezwa, yaani, ng'ombe elfu moja, na kondoo dume elfu moja, na wana-kondoo elfu moja, pamoja na sadaka zao za vinywaji, na dhabihu nyingi kwa ajili ya Israeli wote;


Ndipo Hezekia akajibu, akasema, Sasa mmejifanya wakfu kwa BWANA, karibuni mkalete dhabihu na matoleo ya shukrani nyumbani mwa BWANA. Basi kusanyiko wakaleta dhabihu na matoleo ya shukrani; na wote wenye moyo wa ukarimu, wakaleta sadaka za kuteketezwa.


Na vitu vitakatifu vilikuwa ng'ombe mia sita, na kondoo elfu tatu.


Na tena sadaka za kuteketezwa nazo zilikuwa nyingi, pamoja na mafuta ya sadaka za amani, na sadaka za kinywaji kwa kila sadaka ya kuteketezwa. Hivyo ikatengezeka huduma ya nyumba ya BWANA.


Kisha wakaichinja Pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili, nao makuhani na Walawi wakatahayarika, wakajitakasa, wakaleta sadaka za kuteketezwa nyumbani mwa BWANA.


Na katika kuiweka wakfu nyumba ya Mungu, wakatoa sadaka, ng'ombe mia moja, na kondoo dume mia mbili, na wana-kondoo mia nne; tena wakatoa mbuzi dume kumi na wawili, kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya Waisraeli wote, kwa hesabu ya makabila ya Israeli.


BWANA akamwita Musa, na kusema naye kutoka katika hema ya kukutania, akamwambia,


Ikawa matoleo yake ni sadaka ya kuteketezwa ya ng'ombe, atatoa ng'ombe dume mkamilifu; ataleta mlangoni pa hema ya kukutania, ili akubaliwe mbele ya BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo