Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Mambo ya Nyakati 29:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

22 Basi wakawachinja ng'ombe, na makuhani wakaipokea damu, wakainyunyiza madhabahuni; wakawachinja kondoo dume, na kuinyunyiza damu madhabahuni; wakawachinja na wana-kondoo, na kuinyunyiza damu madhabahuni.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Makuhani walichinja mafahali kwanza, kisha kondoo madume, halafu wanakondoo na kila mara walichukua damu ya wanyama hao na kunyunyiza juu ya madhabahu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Makuhani walichinja mafahali kwanza, kisha kondoo madume, halafu wanakondoo na kila mara walichukua damu ya wanyama hao na kunyunyiza juu ya madhabahu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Makuhani walichinja mafahali kwanza, kisha kondoo madume, halafu wanakondoo na kila mara walichukua damu ya wanyama hao na kunyunyiza juu ya madhabahu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Hivyo wakachinja wale mafahali, nao makuhani wakachukua ile damu na kuinyunyiza kwenye madhabahu, halafu wakawachinja wale kondoo dume saba na kunyunyiza hiyo damu yao kwenye madhabahu, kisha wakawachinja wale wana-kondoo dume na kunyunyiza damu yao kwenye madhabahu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Mambo ya Nyakati 29:22
9 Marejeleo ya Msalaba  

Wakachinja Pasaka, nao makuhani wakamimina damu waliyopokea mikononi mwao, Walawi wakachuna.

Naye atamchinja huyo ng'ombe mbele ya BWANA; kisha wana wa Haruni, hao makuhani, wataileta karibu hiyo damu, na kuinyunyiza damu yake kandokando katika madhabahu iliyo hapo mlangoni pa hema ya kukutania

Kisha nyingine katika hiyo damu ataitia katika pembe za madhabahu iliyo mbele za BWANA, iliyoko ndani ya hema ya kukutania, kisha damu yote ataimwaga hapo chini ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo mlangoni pa hema ya kukutania.

Kisha kuhani atatwaa katika hiyo damu ya sadaka ya kuteketezwa kwa kidole chake na kuitia katika pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, kisha damu yake yote ataimwaga hapo chini ya madhabahu;

Kisha kuhani atatia baadhi ya hiyo damu juu ya pembe za madhabahu ya kufukizia uvumba mzuri mbele ya BWANA iliyo ndani ya hema ya kukutania; kisha damu yote ya huyo ng'ombe ataimwaga hapo chini ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyoko mlangoni pa hema ya kukutania.

Kisha akamchinja; na Musa akainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote.

Kisha akawaleta wana wa Haruni, na Musa akaitia hiyo damu katika ncha za masikio ya upande wa kulia, na katika vidole vya gumba vya mikono yao ya kulia, na katika vidole vya gumba vya maguu yao ya kulia; kisha Musa akainyunyiza hiyo damu katika madhabahu pande zote.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo