Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 26:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

2 Huyo akajenga Elathi, akaurudisha kwa Yuda, baada ya kulala mfalme pamoja na babaze.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Halafu baada ya kifo cha baba yake aliujenga upya mji wa Elothi na kuurudisha kwa Yuda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Halafu baada ya kifo cha baba yake aliujenga upya mji wa Elothi na kuurudisha kwa Yuda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Halafu baada ya kifo cha baba yake aliujenga upya mji wa Elothi na kuurudisha kwa Yuda.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Ndiye aliijenga upya Elathi na kuirudisha kwa Yuda baada ya Amazia kulala na baba zake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Ndiye alijenga upya Elathi kuirudisha kwa Yuda baada ya Amazia kulala pamoja na baba zake.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 26:2
7 Marejeleo ya Msalaba  

Huyo akajenga Elathi, akaurudisha kwa Yuda, baada ya kulala mfalme pamoja na babaze.


Wakati huo Resini mfalme wa Shamu akawarudishia Washami Elathi, akawafukuza Wayahudi kutoka Elathi; nao Washami wakaja Elathi, wakakaa humo hata leo.


Yehoashi mfalme wa Israeli akamtwaa Amazia mfalme wa Yuda, mwana wa Yoashi, mwana wa Ahazia, huko Beth-shemeshi, akamchukua mpaka Yerusalemu, akauvunja ukuta wa Yerusalemu, toka lango la Efraimu mpaka Lango la Pembeni, dhiraa mia nne.


Wakamleta juu ya farasi; wakamzika pamoja na babaze katika mji wa Yuda.


Na watu wote wa Yuda wakamtwaa Uzia, naye alikuwa mwenye miaka kumi na sita, wakamfanya awe mfalme mahali pa Amazia babaye.


Uzia alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala; akatawala huko Yerusalemu miaka hamsini na miwili; na jina la mamaye aliitwa Yekolia wa Yerusalemu.


Ndipo Sulemani akaenda Esion-geberi, na Elothi, pwani ya nchi ya Edomu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo