Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Mambo ya Nyakati 26:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Uzia akakasirika; naye alikuwa na chetezo mkononi cha kufukizia uvumba; naye hapo alipowakasirikia makuhani, ukoma ukamtokea katika paji la uso wake mbele ya makuhani nyumbani mwa BWANA karibu na madhabahu ya kufukizia.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Wakati huo, Uzia alikuwa amesimama hekaluni karibu na madhabahu, ameshikilia chetezo cha kufukizia ubani mkononi. Aliwakasirikia makuhani; na mara alipofanya hivyo, akashikwa na ukoma katika paji la uso wake mbele ya makuhani hao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Wakati huo, Uzia alikuwa amesimama hekaluni karibu na madhabahu, ameshikilia chetezo cha kufukizia ubani mkononi. Aliwakasirikia makuhani; na mara alipofanya hivyo, akashikwa na ukoma katika paji la uso wake mbele ya makuhani hao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Wakati huo, Uzia alikuwa amesimama hekaluni karibu na madhabahu, ameshikilia chetezo cha kufukizia ubani mkononi. Aliwakasirikia makuhani; na mara alipofanya hivyo, akashikwa na ukoma katika paji la uso wake mbele ya makuhani hao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Uzia, aliyekuwa na chetezo mkononi mwake tayari kufukiza uvumba, akakasirika. Alipokuwa anawaghadhibikia makuhani mbele ya madhabahu ya kufukizia uvumba katika Hekalu la Mwenyezi Mungu, ukoma ukamtokea kwenye paji la uso wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Uzia, ambaye alikuwa na chetezo mkononi mwake tayari kufukiza uvumba, akakasirika. Alipokuwa anawaghadhibikia makuhani mbele ya madhabahu ya kufukizia uvumba katika Hekalu la bwana, ukoma ukamtokea penye kipaji chake cha uso.

Tazama sura Nakili

2 Mambo ya Nyakati 26:19
7 Marejeleo ya Msalaba  

Na mfalme aliporudi kutoka Dameski, mfalme akaiona ile madhabahu; mfalme akakaribia madhabahuni, na kutoa sadaka juu yake.

Ndipo Asa akamkasirikia mwonaji, akamtia katika nyumba ya magandalo gerezani, maana amemghadhibikia kwa sababu ya neno hilo. Na wakati uleule Asa akatesa baadhi ya watu.

Ikawa, aliposema naye, mfalme akamwambia, Je! Tumekutia wewe kuwa mshauri wa mfalme? Nyamaza; kwa nini upigwe? Ndipo yule nabii akaacha, akasema, Najua ya kuwa Mungu amekusudia kukuangamiza, kwa sababu umeyafanya haya, wala hukulisikiliza shauri langu.

Azaria kuhani mkuu na makuhani wote wakamtazama, na angalia, alikuwa na ukoma pajini mwa uso, wakamtoa humo upesi; hata na yeye mwenyewe akafanya haraka kutoka, kwa sababu BWANA amempiga.

naye kuhani ataangalia, ikiwa pana uvimbe mweupe katika ngozi yake, na mnywele zimegeuzwa kuwa nyeupe, tena ikiwa panafanyika kidonda katika ule uvimbe,

Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na na kumwona akiwa mwenye ukoma.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo