Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 25:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

27 Basi, toka wakati alipogeuka Amazia katika kumfuata BWANA, wakamfanyia fitina katika Yerusalemu; naye akakimbia mpaka Lakishi; lakini wakatuma kumfuata mpaka Lakishi, wakamwua huko.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Njama za kumuua Amazia zilifanywa Yerusalemu tangu alipomwacha Mwenyezi-Mungu, kwa hiyo alikimbilia Lakishi. Lakini maadui walituma watu Lakishi wakamuua huko.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Njama za kumuua Amazia zilifanywa Yerusalemu tangu alipomwacha Mwenyezi-Mungu, kwa hiyo alikimbilia Lakishi. Lakini maadui walituma watu Lakishi wakamuua huko.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Njama za kumuua Amazia zilifanywa Yerusalemu tangu alipomwacha Mwenyezi-Mungu, kwa hiyo alikimbilia Lakishi. Lakini maadui walituma watu Lakishi wakamuua huko.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Kuanzia wakati Amazia alipogeuka na kuacha kumfuata Mwenyezi Mungu, walipanga njama dhidi yake huko Yerusalemu, naye akakimbilia Lakishi. Lakini wakawatuma watu wamfuatilie huko Lakishi, nao wakamuua huko.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Kuanzia wakati ule Amazia alipogeuka na kuacha kumfuata bwana walifanya shauri baya dhidi yake huko Yerusalemu naye akakimbilia Lakishi, lakini wakawatuma watu wamfuatilie huko Lakishi nao wakamuulia huko.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 25:27
10 Marejeleo ya Msalaba  

Wakafanya fitina juu yake katika Yerusalemu, naye akakimbia mpaka Lakishi, lakini wakatuma watu kumfuata mpaka Lakishi, wakamwua huko.


Adoraimu, Lakishi, Azeka,


naye akatoka ili amlaki Asa, akamwambia, Nisikieni, Ee Asa, na Yuda wote na Benyamini; BWANA yu pamoja nanyi, mkiwa pamoja naye; nanyi mkimtafuta ataonekana kwenu; lakini mkimwacha atawaacha ninyi.


Akamtafuta Ahazia, wakamkamata, (naye alikuwa amejificha Samaria,) wakamleta kwa Yehu, wakamwua; wakamzika, kwa maana wakasema, Huyu ni mwana wa Yehoshafati, huyo aliyemtafuta BWANA kwa moyo wake wote. Wala nyumba ya Ahazia hawakuwa na uwezo wa kuushika ufalme.


Hata walipoondoka kwake, (nao walimwacha ameshikwa sana na maradhi,) watumishi wake mwenyewe wakamfanyia fitina kwa ajili ya damu ya mwana wa Yehoyada kuhani, wakamwua kitandani pake, akafa; wakamzika mjini mwa Daudi, lakini hawakumzika katika makaburi ya wafalme.


Na mambo yote ya Amazia yaliyosalia, ya kwanza hadi mwisho, tazama, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Wafalme wa Yuda na Israeli?


Wakamleta juu ya farasi; wakamzika pamoja na babaze katika mji wa Yuda.


Wakamfanyia fitina watumishi wake, wakamwua katika nyumba yake mwenyewe.


Kisha Yoshua akapita kutoka hapo Libna, na Israeli wote pamoja naye, wakafika Lakishi, wakapiga kambi mbele yake na kupigana nao;


Nao wakawafikia hao wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila la Manase, katika nchi ya Gileadi, na wakasema nao, wakinena,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo