Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 25:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

26 Na mambo yote ya Amazia yaliyosalia, ya kwanza hadi mwisho, tazama, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Wafalme wa Yuda na Israeli?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Matendo mengine yote ya Amazia kutoka mwanzo hadi mwisho yameandikwa katika Kitabu cha Habari za Wafalme wa Yuda na Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Matendo mengine yote ya Amazia kutoka mwanzo hadi mwisho yameandikwa katika Kitabu cha Habari za Wafalme wa Yuda na Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Matendo mengine yote ya Amazia kutoka mwanzo hadi mwisho yameandikwa katika Kitabu cha Habari za Wafalme wa Yuda na Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Amazia, kuanzia mwanzo hadi mwisho, je, hayakuandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na wa Israeli?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Kwa habari ya matukio mengine katika utawala wa Amazia, kuanzia mwanzo hadi mwisho, je, hayakuandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na wa Israeli?

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 25:26
12 Marejeleo ya Msalaba  

Na mambo yake Yeroboamu yaliyosalia, ya kupigana na ya kutawala, tazama, yameandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Israeli.


Na mambo yake Rehoboamu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Yuda?


Basi mambo yote ya Yehoashi yaliyosalia, aliyoyafanya, na ushujaa wake, na jinsi alivyopigana na Amazia mfalme wa Yuda, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Israeli?


Basi habari za mfalme Daudi, mwanzo hadi mwisho, angalia, zimeandikwa katika kumbukumbu za Samweli, mwonaji, na katika kumbukumbu za Nathani, nabii, na katika kumbukumbu za Gadi, mwonaji;


Na mambo yote ya Yehoshafati yaliyosalia, ya kwanza hadi mwisho, angalia, yameandikwa katika salua ya Yehu mwana wa Hanani, iliyotiwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli.


Naye Amazia mwana wa Yoashi mfalme wa Yuda, akaishi miaka kumi na mitano baada ya kufa kwake Yehoashi mwana wa Yehoahazi mfalme wa Israeli.


Basi, toka wakati alipogeuka Amazia katika kumfuata BWANA, wakamfanyia fitina katika Yerusalemu; naye akakimbia mpaka Lakishi; lakini wakatuma kumfuata mpaka Lakishi, wakamwua huko.


Basi mambo yote ya Uzia yaliyosalia, ya kwanza na ya mwisho, aliyaandika Isaya nabii, mwana wa Amozi.


Na mambo yote ya Yothamu yaliyosalia, na vita vyake vyote, na njia zake, tazama, yameandikwa katika Kitabu cha Wafalme wa Israeli na Yuda.


Basi mambo yote ya Hezekia yaliyosalia, na matendo yake mema, tazama, yameandikwa katika maono ya nabii Isaya, mwana wa Amozi, katika Kitabu cha Wafalme wa Yuda na Israeli.


na mambo yake, ya kwanza hadi ya mwisho, tazama, yameandikwa katika Kitabu cha Wafalme wa Israeli na Yuda.


Basi mambo yote ya Yehoyakimu yaliyosalia, na machukizo yake aliyoyafanya, nayo yaliyoonekana kwake, tazama, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda; na Yekonia mwanawe akatawala mahali pake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo