Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 24:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

7 Kwa kuwa wana wa Athalia, yule mwanamke mwovu, walikuwa wameibomoa nyumba ya Mungu; na vitakatifu vyote vya nyumba ya BWANA wamewapatia Mabaali.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 (Athalia yule mwanamke mwovu na wafuasi wake walivunja nyumba ya Mungu na kuingia ndani; na vyombo vitakatifu vya nyumba ya Mwenyezi-Mungu walivitumia katika ibada za Mabaali.)

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 (Athalia yule mwanamke mwovu na wafuasi wake walivunja nyumba ya Mungu na kuingia ndani; na vyombo vitakatifu vya nyumba ya Mwenyezi-Mungu walivitumia katika ibada za Mabaali.)

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 (Athalia yule mwanamke mwovu na wafuasi wake walivunja nyumba ya Mungu na kuingia ndani; na vyombo vitakatifu vya nyumba ya Mwenyezi-Mungu walivitumia katika ibada za Mabaali.)

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Kwa kuwa wana wa yule mwanamke mwovu Athalia, walikuwa wamevunja na kuingia katika Hekalu la Mungu, nao wakawa wamevitumia hata vile vitu vilivyowekwa wakfu kwa Mwenyezi Mungu kwa mabaali.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Kwa kuwa wana wa yule mwanamke mwovu Athalia, walikuwa wamevunja na kuingia katika Hekalu la Mungu, nao wakawa wamevitumia hata vile vitu vilivyowekwa wakfu kwa bwana kwa mabaali.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 24:7
18 Marejeleo ya Msalaba  

Na Athalia, mama yake Ahazia, alipoona ya kuwa mwanawe amekufa, akainuka, akawaharibu wazao wote wa kifalme.


Yoashi akawaambia makuhani, Fedha yote ya vitu vitakatifu iliyoletwa nyumbani mwa BWANA, fedha ya matumizi, fedha ya watu kadiri alivyoandikiwa kila mtu, na fedha yote iliyoletwa kama mtu yeyote aonavyo moyoni mwake kuileta nyumbani mwa BWANA,


nao wakakwea juu ya Yuda, wakaipenya, wakaichukua mali yote iliyoonekama nyumbani mwa mfalme, na wanawe pia, na wakeze; asibakizwe mtoto hata mmoja, ila Ahazia, aliyekuwa mdogo miongoni mwa wanawe.


Yeye naye akazifuata njia za nyumba ya Ahabu; kwa kuwa mamaye alikuwa mshauri wake katika kufanya maovu.


Ikawa baada ya haya, Yoashi alikuwa na nia ya kuitengeneza nyumba ya Mungu.


Esta akasema, Ni mtesi, tena ni adui, ndiye huyu Hamani, mtu mbaya kabisa. Mara Hamani akaingiwa na hofu mbele ya mfalme na malkia.


Kuwakumbuka wenye haki huwa na baraka; Bali jina la mtu mwovu litaoza.


Bali umejiinua juu ya Bwana wa mbingu; nao wamevileta vyombo vya nyumba yake mbele yako; na wewe, na wakuu wako, na wake zako, na masuria wako, mmevinywea; nawe umeisifu miungu ya fedha na ya dhahabu na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe; wasioona, wala kusikia, wala kujua neno lolote; na Mungu yule, ambaye pumzi yako i mkononi mwake, na njia zako zote ni zake, hukumtukuza.


Na sasa nitaifunua aibu yake mbele ya macho ya wapenzi wake, wala hapana mtu atakayemwokoa katika mkono wangu.


Nami nitamwadhibu kwa sababu ya siku za Mabaali, aliowafukizia uvumba; hapo alipojipamba kwa pete masikioni mwake, na kwa vito asema BWANA.


Hapo ndipo atakapofunuliwa yule mwasi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa dhihirisho la kuja kwake;


Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.


Wana wa Israeli walifanya mambo maovu mbele za macho ya BWANA, na wakawatumikia Mabaali.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo