2 Mambo ya Nyakati 24:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC
27 Basi kwa habari ya wanawe, na ukubwa wa mizigo aliolemewa, na majengo ya nyumba ya Mungu, tazama, hayo yameandikwa katika maelezo ya kitabu cha Wafalme. Na Amazia mwanawe akatawala mahali pake.
27 Habari za wanawe Yoashi za kuirekebisha nyumba ya Mwenyezi-Mungu na unabii wote juu yake, zimeandikwa katika Maelezo ya Kitabu cha Wafalme. Amazia mwanawe alitawala baada yake.

27 Kwa habari za wanawe, unabii mwingi kumhusu na kumbukumbu za kutengenezwa upya kwa Hekalu la Mungu, zimeandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme. Amazia mwanawe akawa mfalme baada yake.
27 Kwa habari za wanawe, unabii mwingi kumhusu na kumbukumbu za kutengenezwa upya kwa Hekalu la Mungu, zimeandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme. Amazia mwanawe akawa mfalme baada yake.
Yoashi mfalme wa Yuda akavitwaa vyote alivyoviweka wakfu Yehoshafati, na Yehoramu, na Ahazia, baba zake, wafalme wa Yuda, navyo vyote alivyoweka wakfu mwenyewe, na dhahabu yote iliyoonekana katika hazina za nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme, akamletea Hazaeli mfalme wa Shamu; basi akaenda zake kutoka Yerusalemu.
Kwa maana Yozakari mwana wa Shimeathi, na Yehozabadi mwana wa Shomeri, watumishi wake, wakampiga, naye akafa; wakamzika pamoja na babaze mjini mwa Daudi. Na Amazia mwanawe akatawala mahali pake.
Na mambo yote ya Yehoshafati yaliyosalia, ya kwanza hadi mwisho, angalia, yameandikwa katika salua ya Yehu mwana wa Hanani, iliyotiwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli.
Na mfalme na Yehoyada waliwapa hao waliofanya kazi ya utumishi wa nyumba ya BWANA; nao wakawaajiri waashi na maseremala ili kuitengeza nyumba ya BWANA, na hao pia wafuao chuma na shaba ili kuitengeza nyumba ya BWANA.
Amazia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka ishirini na tisa; na jina la mamaye aliitwa Yehoadani wa Yerusalemu.
Basi mambo yake Sulemani yaliyosalia, tangu mwanzo hadi mwisho je! Hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu la Nathani nabii, katika unabii wa Ahiya, Mshiloni, na katika maono ya Ido mwonaji ambayo yahusu Yeroboamu mwana wa Nebati?