Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 24:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

20 Na Roho ya Mungu ikamjia Zekaria, mwana wa Yehoyada, kuhani; naye akasimama mbele ya watu palikuwa juu, akawaambia, Mungu asema hivi, Kwa nini ninyi mnazivunja amri za BWANA, hata msiweze kufanikiwa? Kwa kuwa mmemwacha BWANA, yeye naye amewaacha ninyi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Ndipo Roho ya Mungu ikamjia Zekaria mwana wa kuhani Yehoyada, naye akasimama mbele ya watu mahali palipokuwa juu kidogo, akawaambia, “Mwenyezi-Mungu aliwaulizeni kwa nini mnazivunja amri zake na sasa hamwezi kufanikiwa! Kwa vile mmemwacha, naye pia amewaacha!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Ndipo Roho ya Mungu ikamjia Zekaria mwana wa kuhani Yehoyada, naye akasimama mbele ya watu mahali palipokuwa juu kidogo, akawaambia, “Mwenyezi-Mungu aliwaulizeni kwa nini mnazivunja amri zake na sasa hamwezi kufanikiwa! Kwa vile mmemwacha, naye pia amewaacha!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Ndipo Roho ya Mungu ikamjia Zekaria mwana wa kuhani Yehoyada, naye akasimama mbele ya watu mahali palipokuwa juu kidogo, akawaambia, “Mwenyezi-Mungu aliwaulizeni kwa nini mnazivunja amri zake na sasa hamwezi kufanikiwa! Kwa vile mmemwacha, naye pia amewaacha!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Ndipo Roho wa Mwenyezi Mungu akaja juu ya Zekaria mwana wa Yehoyada kuhani. Akasimama mbele ya watu akasema, “Hili ndilo asemalo Mungu, ‘Kwa nini mnakataa kuzitii amri za Mwenyezi Mungu? Hamtafanikiwa kwa kuwa mmemwacha Mwenyezi Mungu, naye amewaacha ninyi.’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Ndipo Roho wa bwana akaja juu ya Zekaria mwana wa Yehoyada kuhani. Akasimama mbele ya watu akasema, “Hili ndilo asemalo Mungu, ‘Kwa nini mnakataa kuzitii amri za bwana? Hamtafanikiwa kwa kuwa mmemwacha bwana, yeye naye amewaacha ninyi.’ ”

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 24:20
24 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo roho ikamjia Abishai, mkuu wa wale thelathini, naye akasema, Sisi tu watu wako, Ee Daudi; Na wa upande wako, Ee mwana wa Yese; Amani, naam, amani iwe kwako, Na amani iwe kwao wakusaidiao; Maana Mungu wako ndiye akusaidiye. Ndipo Daudi akawakaribisha, akawaweka wawe makamanda wa kile kikosi.


Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA huchunguza mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, atakuwa nawe; ukimwacha, atakutupa milele.


Ndipo akaja Shemaya nabii kwa Rehoboamu, na kwa wakuu wa Yuda, waliokusanyika Yerusalemu kwa sababu ya Shishaki, akawaambia, BWANA asema hivi, Ninyi mmeniacha mimi, kwa hiyo nami nimewaacha ninyi mkononi mwa Shishaki.


Ndipo Yahazieli mwana wa Zekaria, mwana wa Benaya, mwana wa Yeieli, mwana wa Matania, Mlawi, wa wana wa Asafu, akajiliwa na Roho ya BWANA, katikati ya kusanyiko;


Ndipo wakamleta nje mwana wa mfalme, wakamvika taji, na kumpa ule ushuhuda, wakamtawaza kuwa mfalme; Yehoyada na wanawe wakamtia mafuta, wakasema, Mfalme na aishi.


Maana wakaja jeshi la Washami watu wachache; BWANA akatia mikononi mwao jeshi kubwa mno, kwa sababu wamemwacha BWANA, Mungu wa baba zao. Hivyo wakamfanyia Yoashi hukumu.


Ikawa, aliposema naye, mfalme akamwambia, Je! Tumekutia wewe kuwa mshauri wa mfalme? Nyamaza; kwa nini upigwe? Ndipo yule nabii akaacha, akasema, Najua ya kuwa Mungu amekusudia kukuangamiza, kwa sababu umeyafanya haya, wala hukulisikiliza shauri langu.


Kwa hiyo hasira ya BWANA imekuwa juu ya Yuda na Yerusalemu, naye amewatoa kuwa matetemeko, wawe ushangao, na mazomeo, kama muonavyo kwa macho yenu.


Uovu wako mwenyewe utakurudi, maasi yako yatakukaripia; ujue, basi, ukaone, ya kuwa ni jambo baya sana na uchungu, kuwa umemwacha BWANA, Mungu wako, na ya kuwa moyoni mwako hamna kunihofu, asema Bwana, BWANA wa majeshi.


BWANA asema hivi, Simama katika uwanja wa nyumba ya BWANA, useme na miji yote ya Yuda, wajao ili kuabudu katika nyumba ya BWANA; sema nao maneno yote ninayokuamuru kuwaambia, usizuie hata neno moja.


Njia yako na matendo yako yamekupatia haya; huu ndio uovu wako; kwa maana ni uchungu, hakika unafikia hata moyo wako.


Tena itakuwa mtakapouliza, BWANA ametutenda mambo hayo yote kwa sababu gani? Ndipo utakapowaambia, Vile vile kama ninyi mlivyoniacha mimi, na kuwatumikia miungu mingine katika nchi yenu wenyewe, ndivyo mtakavyowatumikia wageni katika nchi isiyo yenu.


Maovu yenu yameyageuza haya, na dhambi zenu zimewazuilia mema msiyapate.


Wao humchukia yeye akemeaye langoni, nao humzira anenaye maneno ya adili.


Musa akawaambia, Kwa nini ninyi sasa kuyakaidi maagizo ya BWANA? Maana halitafanikiwa jambo hilo.


hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya Zakaria mwana wa Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu.


tangu damu ya Habili hata damu ya Zakaria, aliyeuawa kati ya madhabahu na hekalu. Naam, nawaambieni ya kwamba itatakwa kwa kizazi hiki.


Ndipo hasira yangu itakapowaka juu yao siku hiyo, nami nitawaacha, nitawaficha uso wangu, nao wataliwa, tena watajiliwa na mambo maovu mengi na mashaka; hata waseme siku hiyo, Je! Kujiliwa kwetu na maovu haya si kwa sababu Mungu wetu hayumo kati yetu?


Lakini Roho ya BWANA ikamjia juu yake Gideoni; naye akapiga tarumbeta; na Abiezeri walikutanika na kumfuata.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo