Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 24:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Hata hivyo akawatuma manabii, ili kuwarudisha kwa BWANA; nao wakawashuhudia; lakini hawakukubali kuwasikiliza.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Hata hivyo, aliwapelekea manabii kuwaonya ili wamrudie Mwenyezi-Mungu, lakini wao hawakuwasikiliza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Hata hivyo, aliwapelekea manabii kuwaonya ili wamrudie Mwenyezi-Mungu, lakini wao hawakuwasikiliza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Hata hivyo, aliwapelekea manabii kuwaonya ili wamrudie Mwenyezi-Mungu, lakini wao hawakuwasikiliza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Ingawa Mwenyezi Mungu aliwatuma manabii wawarudishe watu kwake na ingawa waliwaonya, hawakuwasikiliza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Ingawa bwana aliwatuma manabii wawarudishe watu kwake na ingawa waliwaonya, hawakuwasikiliza.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 24:19
23 Marejeleo ya Msalaba  

Tena akamwasi mfalme Nebukadneza, aliyemwapisha kwa Mungu; lakini akajifanyia shingo ngumu, akajitia moyo nguvu asimgeukie BWANA, Mungu wa Israeli.


Walakini hawakukutii, wakakuasi, wakaitupa sheria yako nyuma yao, wakawaua manabii wako waliowaonya ili wapate kukurudia wewe; wakakufuru sana.


Lakini miaka mingi ukachukuliana nao, nawe ukawashuhudia kwa roho yako kwa vinywa vya manabii wako; wao wasitake kusikiliza; kwa hiyo ukawatia katika mikono ya watu wa nchi.


Tegeni masikio, sikieni sauti yangu, sikilizeni mkasikie neno langu.


Ni nani miongoni mwenu atakayetega sikio lake kuyasikia hayo? Atakayesikiliza na kusikia kwa wakati ujao?


Nisikilizeni mimi, enyi watu wangu; nisikieni, taifa langu; maana sheria itatoka kwangu, na kutoa haki yangu iwe nuru ya mataifa.


Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi; Nami nitafanya nanyi agano la milele, Naam, rehema za Daudi zilizo imara.


Tangu mwaka wa kumi na tatu wa kutawala kwake Yosia, mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda, hata siku hii ya leo, miaka hii ishirini na mitatu, neno la BWANA limenijia, nami nimesema nanyi, nikiamka mapema na kusema; lakini ninyi hamkusikiliza.


Lakini ninyi hamkunisikiliza, asema BWANA; ili mnikasirishe kwa kazi ya mikono yenu, na kujidhuru nafsi zenu.


Basi BWANA wa majeshi asema hivi, Kwa kuwa hamkuyasikiliza maneno yangu,


kuyasikiliza maneno ya watumishi wangu, manabii, ninaowatuma kwenu, naam, nikiondoka mapema na kuwatuma; lakini ninyi hamkuwasikiliza;


Msiwe ninyi kama baba zenu, ambao manabii wa zamani waliwalilia, wakisema, BWANA wa majeshi asema hivi, Rudini sasa, na kuziacha njia zenu mbovu, na matendo yenu maovu; lakini hawakusikia, wala kunitii, asema BWANA.


Mwenye masikio na asikie.


Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishika hata mtu akifufuka katika wafu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo