Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 24:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 Wakaiacha nyumba ya BWANA, Mungu wa baba zao; wakatumikia Maashera na sanamu; ghadhabu ikawajia Yuda na Yerusalemu kwa sababu ya hiyo hatia yao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Basi, watu wakaacha kuabudu katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao, wakaanza kuabudu Maashera na sanamu. Ghadhabu ya Mungu iliwaka juu ya Yuda na Yerusalemu kwa sababu ya hatia hii.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Basi, watu wakaacha kuabudu katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao, wakaanza kuabudu Maashera na sanamu. Ghadhabu ya Mungu iliwaka juu ya Yuda na Yerusalemu kwa sababu ya hatia hii.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Basi, watu wakaacha kuabudu katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao, wakaanza kuabudu Maashera na sanamu. Ghadhabu ya Mungu iliwaka juu ya Yuda na Yerusalemu kwa sababu ya hatia hii.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Wakaacha Hekalu la Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao, wakaabudu nguzo za maashera na sanamu. Kwa sababu ya hatia yao, hasira ya Mungu ikawajia Yuda na Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Wakaacha Hekalu la bwana, Mungu wa baba zao, wakaabudu nguzo za maashera na sanamu. Kwa sababu ya hatia yao, hasira ya Mungu ikawajia Yuda na Yerusalemu.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 24:18
28 Marejeleo ya Msalaba  

Tena hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israeli, akamchochea Daudi juu yao, akisema, Nenda, ukawahesabu watu wa Israeli na Yuda.


Maana hao pia wakajijengea mahali pa juu, na nguzo, na maashera, juu ya kila kilima kirefu, na chini ya kila mti wenye majani mabichi.


lakini umekosa kuliko wote waliokutangulia, umekwenda kujifanyia miungu mingine, na sanamu zilizoyeyuka, unikasirishe, na kunitupa nyuma yako;


Ikawa ulipothibitika ufalme wa Rehoboamu, naye amepata nguvu, aliiacha Torati ya BWANA, na Israeli wote pamoja naye.


Ikawa katika mwaka wa tano wa mfalme Rehoboamu, akapanda Shishaki, mfalme wa Misri, juu ya Yerusalemu; kwa kuwa walikuwa wamemwasi BWANA;


Yehu mwana wa Hanani mwonaji akatoka kwenda kumlaki, akamwambia mfalme Yehoshafati, Je! Imekupasa kuwasaidia waovu, na kuwapenda wamchukiao BWANA? Kwa ajili ya hayo ghadhabu itokayo kwa BWANA i juu yako.


lakini umeiendea njia ya wafalme wa Israeli, ukawaongoza Yuda na wakazi wa Yerusalemu kwenye kukosa uaminifu, kama walivyofanya nyumba ya Ahabu; tena umewaua ndugu zako wa nyumba ya baba yako, waliokuwa wema kuliko wewe;


Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA kama nyumba ya Ahabu; kwa kuwa hao walikuwa washauri wake, baada ya kifo cha baba yake, hata aangamie.


Hata baada ya kufa kwake Yehoyada, wakuu wa Yuda wakamwendea mfalme, wakamsujudia. Naye mfalme akawasikiliza maneno yao.


Ikawa baada ya haya, Yoashi alikuwa na nia ya kuitengeneza nyumba ya Mungu.


Kwa hiyo hasira ya BWANA ikawaka juu ya Amazia, akamtuma kwake nabii, aliyemwambia, Mbona umeitafuta miungu ya watu, isiyowaokoa watu wao mkononi mwako?


wakawaambia, Hamtawaleta wafungwa humo; kwa sababu mnayanuia yatakayotutia hatiani mbele za BWANA, kuongeza dhambi zetu, na hatia yetu; maana hatia yetu ni kubwa, na ghadhabu kali ipo juu ya Israeli.


Kwa hiyo hasira ya BWANA imekuwa juu ya Yuda na Yerusalemu, naye amewatoa kuwa matetemeko, wawe ushangao, na mazomeo, kama muonavyo kwa macho yenu.


Walakini Hezekia hakuwa na shukrani kadiri alivyofadhiliwa; kwa kuwa moyo wake ulijawa na kiburi; kwa hiyo ikawako hasira juu yake, na juu ya Yuda na Yerusalemu.


kwa sababu wameniacha mimi, na kuifukizia uvumba miungu mingine, ili wanikasirishe mimi kwa matendo yote ya mikono yao; kwa hiyo ghadhabu yangu imemwagika juu ya mahali hapa, wala isizimike.


Ujihadhari nafsi yako, usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi ile unayoiendea, lisiwe mtego katikati yako.


Bali utabomoa madhabahu zao, na kuvunjavunja nguzo zao, na kuyakatakata maashera yao.


na wakati huo watoto wao wazikumbuka madhabahu zao, na maashera yao, karibu na miti yenye majani mabichi juu ya milima mirefu.


Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efraimu, na kama mwanasimba kwa nyumba ya Yuda; mimi, naam, mimi nitararua, kisha nitakwenda zangu; nitachukua mbali, wala hapatakuwa na mtu wa kuokoa.


Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi.


Je! Huyo Akani mwana wa Zera hakukosa katika vile vitu vilivyowekwa wakfu, na hasira ikauangukia mkutano wote wa Israeli? Kisha mtu huyo hakuangamia peke yake katika uovu wake?


Walichagua miungu mipya, Ndipo kulikuwa na vita malangoni; Je! Ilionekana ngao au mkuki Katika watu elfu arubaini wa Israeli?


Kisha ikawa, mara alipokufa Gideoni, wana wa Israeli wakakengeuka tena, wakawaandama Mabaali kwa ukahaba, wakamfanya Baal-berithi kuwa ni mungu wao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo