Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Mambo ya Nyakati 24:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

15 Lakini Yehoyada akawa mzee, mwenye siku nyingi, akafa; alipokufa alikuwa na umri wa miaka mia moja na thelathini.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Lakini Yehoyada alizeeka na alipofikisha umri wa miaka 130, alifariki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Lakini Yehoyada alizeeka na alipofikisha umri wa miaka 130, alifariki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Lakini Yehoyada alizeeka na alipofikisha umri wa miaka 130, alifariki.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Basi Yehoyada alikuwa mzee aliyeshiba siku alipofariki. Alikufa akiwa na umri wa miaka mia moja na thelathini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Basi Yehoyada alikuwa mzee aliyeshiba siku wakati alipofariki. Alikufa akiwa na umri wa miaka 130.

Tazama sura Nakili




2 Mambo ya Nyakati 24:15
10 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema.


Abrahamu akafariki, naye akafa katika uzee mwema, mzee sana, ameshiba siku, akakusanyika kwa watu wake.


Yakobo akamjibu Farao, Siku za kuishi kwangu ni miaka mia moja na thelathini; siku za maisha yangu zimekuwa chache, tena za taabu, wala hazikufikia siku za maisha ya baba zangu katika siku za kuishi kwao.


Basi Daudi alipokuwa mzee kwa kuishi siku nyingi; alimtawaza mwanawe Sulemani awe mfalme wa Waisraeli.


Nao walipomaliza, wakaleta mbele ya mfalme na Yehoyada fedha iliyobaki, na kwavyo vikafanywa vyombo vya nyumba ya BWANA, vyombo vya utumishi, navyo vya kutolea, na miiko, na vyombo vya dhahabu na fedha. Wakatoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya BWANA, mara kwa mara, siku zote za Yehoyada.


Wakamzika katika mji wa Daudi kati ya wafalme, kwa sababu ametenda mema katika Israeli, na kwa Mungu, na katika nyumba yake.


Yehoyada akamwoza wake wawili, naye akazaa watoto wa kiume na wa kike.


Utafika kaburini mwenye umri mtimilifu, Kama mganda wa ngano ulivyo wakati wake.


Miaka ya maisha yetu ni sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Tena kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana wakati unapita upesi nasi kutokomea punde.


Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonesha wokovu wangu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo