Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

2 Mambo ya Nyakati 24:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

12 Na mfalme na Yehoyada waliwapa hao waliofanya kazi ya utumishi wa nyumba ya BWANA; nao wakawaajiri waashi na maseremala ili kuitengeza nyumba ya BWANA, na hao pia wafuao chuma na shaba ili kuitengeza nyumba ya BWANA.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Mfalme na Yehoyada walizitoa fedha hizo na kuwapa wale waliosimamia kazi ya urekebishaji wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Nao wakawaajiri waashi, maseremala warekebishe nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Waliajiri pia mafundi wa chuma na shaba ili kurekebisha nyumba ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Mfalme na Yehoyada walizitoa fedha hizo na kuwapa wale waliosimamia kazi ya urekebishaji wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Nao wakawaajiri waashi, maseremala warekebishe nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Waliajiri pia mafundi wa chuma na shaba ili kurekebisha nyumba ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Mfalme na Yehoyada wakawapa wale watu waliofanya kazi iliyotakiwa katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. Wakawaajiri waashi na maseremala ili kutengeneza Hekalu la Mwenyezi Mungu, pia wafanyakazi za chuma na shaba ili kukarabati Hekalu la Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Mfalme na Yehoyada wakawapa wale watu waliofanya kazi iliyotakiwa katika Hekalu la bwana. Wakawaajiri waashi na maseremala ili kutengeneza Hekalu la bwana, pia wafanyakazi za chuma na shaba ili kukarabati Hekalu la bwana.

Tazama sura Nakili

2 Mambo ya Nyakati 24:12
7 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha Hiramu, mfalme wa Tiro, akatuma wajumbe kwa Daudi, akampelekea na mierezi, na maseremala, na waashi; nao wakamjengea Daudi nyumba.

Sulemani alikuwa na wapagazi elfu sabini na wakatao miti milimani elfu themanini;

Ikawa wakati walipoletewa kasha wasimamizi wa mfalme kwa mkono wa Walawi, nao wakaona ya kwamba kuna fedha nyingi, huja karani wa mfalme, na msimamizi wake kuhani mkuu, wakatoa yaliyomo kashani, kisha hulichukua kasha, na kulirudisha mahali pake. Ndivyo walivyofanya siku kwa siku, wakakusanya fedha tele.

Hivyo mafundi wakafanya kazi yao, nao wakaimaliza, wakaisimamisha nyumba ya Mungu kama ilivyopasa, wakaifanya imara.

Basi kwa habari ya wanawe, na ukubwa wa mizigo aliolemewa, na majengo ya nyumba ya Mungu, tazama, hayo yameandikwa katika maelezo ya kitabu cha Wafalme. Na Amazia mwanawe akatawala mahali pake.

Hata katika mwaka wa kumi na nane wa kutawala kwake, alipokwisha kuisafisha nchi, na nyumba, akamtuma Shafani, mwana wa Azalia, na Maaseya, mkuu wa mji, na Yoa, mwana wa Yoahazi, mwandishi wa kumbukumbu, waitengeneze nyumba ya BWANA, Mungu wake.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo