Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Mambo ya Nyakati 23:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 Yehoyada akauamuru usimamizi wa nyumba ya BWANA chini ya mkono wa makuhani Walawi, aliowagawa Daudi nyumbani mwa BWANA, ili wazisongeze sadaka za kuteketezwa za BWANA, kama ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, kwa kufurahi na kuimba, kama alivyoamuru Daudi.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Kuhani Yehoyada akaweka walinzi kulinda nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Hao walinzi walisimamiwa na makuhani na Walawi ambao Daudi aliwaweka katika huduma ya kutunza nyumba ya Mwenyezi-Mungu na kutoa sadaka za kuteketezwa kwa Mwenyezi-Mungu kama ilivyoandikwa katika sheria ya Mose, wakishangilia na kuimba kwa kufuata amri ya Daudi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Kuhani Yehoyada akaweka walinzi kulinda nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Hao walinzi walisimamiwa na makuhani na Walawi ambao Daudi aliwaweka katika huduma ya kutunza nyumba ya Mwenyezi-Mungu na kutoa sadaka za kuteketezwa kwa Mwenyezi-Mungu kama ilivyoandikwa katika sheria ya Mose, wakishangilia na kuimba kwa kufuata amri ya Daudi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Yehoyada akaweka uangalizi wa Hekalu la Mwenyezi Mungu mikononi mwa makuhani, hao Walawi, ambao Mfalme Daudi alikuwa amewagawa ili wahudumu hekaluni kwa ajili ya kutoa sadaka za kuteketezwa za Mwenyezi Mungu, kama ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, kwa kushangilia na kuimba, vile Daudi alikuwa ameagiza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Kisha Yehoyada akaweka uangalizi wa Hekalu la bwana mikononi mwa makuhani, waliokuwa Walawi, ambao Mfalme Daudi alikuwa amewagawa ili wahudumu hekaluni kwa ajili ya kutoa sadaka za kuteketezwa za bwana kama ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, kwa kushangilia na kuimba kama Daudi alivyokuwa ameagiza.

Tazama sura Nakili

2 Mambo ya Nyakati 23:18
13 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa Daudi alisema, BWANA, Mungu wa Israeli, amewastarehesha watu wake; naye hukaa Yerusalemu milele;

Akawasimamisha Walawi nyumbani mwa BWANA wenye matoazi, wenye vinanda, na wenye vinubi, kama alivyoamuru Daudi, na Gadi mwonaji wa mfalme, na Nathani nabii; kwani BWANA aliamuru hivi kwa manabii wake.

Hezekia akaamuru kutoa sadaka ya kuteketezwa madhabahuni. Na wakati ilipoanza sadaka hiyo ya kuteketezwa, ukaanza na huo wimbo wa BWANA, na parapanda, pamoja na vinanda vya Daudi mfalme wa Israeli.

Tena Hezekia mfalme na wakuu wakawaamuru Walawi, wamwimbie BWANA sifa kwa maneno ya Daudi, na ya Asafu mwonaji. Wakaimba sifa kwa furaha, wakainamisha vichwa, wakaabudu.

Ndipo wakasimama makuhani Walawi, wakawabariki watu; ikasikiwa sauti yao, sala yao ikafika hata makao yake matakatifu, yaani, mbinguni.

Akawaweka makuhani katika kazi zao, akawatia moyo kutumika katika nyumba ya BWANA.

Wakalipandisha sanduku, na ile hema ya kukutania, na vyombo vitakatifu vyote vilivyokuwamo Hemani, vitu hivyo makuhani Walawi wakavipandisha.

Makuhani wakasimama kwenye nafasi zao walipoagizwa; Walawi nao pamoja na vinanda vya BWANA, alivyovifanya Daudi mfalme, ili kumshukuru BWANA, kwa maana fadhili zake ni za milele, hapo aliposifu Daudi kwa mikono yao; nao makuhani wakapiga panda mbele yao; nao Israeli wote wakasimama.

wakaifanya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu kwa furaha, kwa muda wa siku saba; kwa kuwa BWANA amewafurahisha, na kumgeuza moyo mfalme wa Ashuru, awaelekee, ili awatie nguvu mikono yao katika kazi hiyo ya nyumba ya Mungu, Mungu wa Israeli.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo